mtunzasiri
JF-Expert Member
- Dec 24, 2012
- 1,449
- 993
Sure. Hata mm ndugu yangu alinitumia BB Storm ilikuwa na contract ya Verizon Wireless. HApa kwetu Bongo ikashindwa Kufanya kazi kwenye neti na Kurechaji Credit. hadi nlipokutana na Jamaangu alikuwa akijulikana kwa jina la Gadget Master. Alikuwa na Uwezo wa ajabu kugundua Matatizo ya Simu/pc na kusolve. Ila kwa sasa jamaa yuko india anapiga mambo ya programming.
Kwa ufupi. Aliiflash na kuifanyia firmware nyingine kitu kikaenda hewani. Bei alinichaji 20.
Labda jaribu pale SApna nliwahi kusikia wanashughulika na hayo Mambo pia.
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
nipo Singida na nilinunua cm kama hiyo Tigo Arusha hadi leo inanisumbua,nimewapelekea mafundi kama wawili wameshindwa kuifungua.Naomba mnielekeze hapo sapna nikija Dar niwatembelee wandugu
Hujawahi fika dar enh?? Mbado??
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Nimefika ila hiyo sehemu siifahamu ndugu.Nielekeze au ndo ushanifanya mshamba!
Sapna iko maeneo ya posta. Wakt unatokea upande wa posta mpya kule iliko benk ya crdb na nmb. Ukifka mbele kuna keepleft pale. Kuna barabara iko mkono wako wa kulia. Zko mbili pale. Fata ile ambayo iko oposite na benk ya tanzania posta benk. Yani unaacha njia inayoshuka upande wa chini na ile inayokwenda upande wa kule ktk bahari ambapo ipo bank ya nbc. Kulia kwako ndo kuna hzo barabara mbili. Ndo utafata ile ambayo inakwenda oposite na tanzania posta bank.
Mi mwenyewe nipo singida. Kama vip ukiwa tyr nitafute nikuelekeze au kama utakuwa dar nitakupeleka