Msaada unahitajika

Ngereja

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
798
333
Ninaomba msaada kwa anayefahamu. Laptop yangu kuanzia jana nikiiwasha inaanza na pop-up window message "Found New Hardware Wizard", ilihali sijaweka hardware yoyote mpya. Je ni tatizo gani?. Ninatumia Microsoft Windows XP Professional SP3.

Hapo kabla kuna kirusi "autorun.inf" alinishambulia lakini nilifanikiwa kumuondoa, je yawezekana hajaondoka kabisa? pia naomba msaada wa namna ya kuondoa traces zote za "autorun.inf" kutoka kwenye registry manually

Ahsanteni kwa msaada utakaotolewa.
 
Angalia uzuri kuna thread na maelezo ya jinsi ya kuondoa autorun kingine ukitumia avast pro ver 4.8 na kuendelea ukinstall na kufanya update unaweza kufanya boot scan itaondoa hiyo autorun .

Pili kuhusu suala lako la new hardware inawezekana wakati una scan au kufanya kitu kuna driver imeondoka au ina hitaji updates angalia vizuri na kama unatumia antivirus kama norton huwa ina tabia hiyo files fulani fulani zikiwa corrupt

mchana mwema
 
Ninaomba msaada kwa anayefahamu. Laptop yangu kuanzia jana nikiiwasha inaanza na pop-up window message "Found New Hardware Wizard", ilihali sijaweka hardware yoyote mpya. Je ni tatizo gani?. Ninatumia Microsoft Windows XP Professional SP3.

Hapo kabla kuna kirusi "autorun.inf" alinishambulia lakini nilifanikiwa kumuondoa, je yawezekana hajaondoka kabisa? pia naomba msaada wa namna ya kuondoa traces zote za "autorun.inf" kutoka kwenye registry manually

Ahsanteni kwa msaada utakaotolewa.

Inavyoonekana hapo kwa harakaharaka ni hao virus watakuwa wameondoka na files za driver ndo maana inaoneka kuna hardware mpya ilhali haujaweka hardware mpya.

Re-install window au tafuta hiyo hardware mpya iliyo ongezeka katika device manager then udownload driver.
pole
 
Ahasanteni, ni kweli nimeenda kwenye device managers nikakuta kuna "other devices" mbili zina yellow ? hazifanyi kazi, najaribu ku-check kujua ni hardware gani, ila kwenye details za kila hardware kuna information zifuatazo:

1. ROOT\LEGACY_AVGIO\0000
2. ROOT\LEGACY_AVGNTFL\0000

Naweza ku-disable au kuziondoa kabisa kama sio za muhimu
Naweza kupata interpretation ya 1 & 2 hapo juu?

Ahasanteni tena kwa msaada wenu.
 
Back
Top Bottom