Hebu twende polepole kwanza!
Kwanini wewe utume na uwatumie jamaa zako picha za X kwenye simu yako? Wewe si umeoa?!, sasa kwenye hayo mapicha unatafuta nini? Kama ulikuwa bado unataka kuangalia hayo mapicha kwanini ulikimbilia kuoa? Kwani wewe ukigundua kuwa mkeo anatumiwa au anatuma mapicha ya X kwa wengine utaridhika? Yaani ufanye wewe iwe sawa, lakini akifanya yeye si sawa!, kisa wewe ni mwanaume?! Unamlaumu mkeo kwa kutuma picha za X kwa ndugu zako, let's say ni sawa kwamba ni kitu kitu kibaya! Lakini asingezikuta hizo picha kwenye simu yako angekuwa na cha kutuma!!?? Kwa hiyo yote haya ni wewe uliyeyasababisha, usingekuwa na hizo picha kesi ya kukulaumu au hata ya kutuma kwa ndugu isingekuwepo.
Unaogopa nini mkeo akiangalia simu yako? unaficha nini ambacho hutaki mkeo akione? Kama umeoa na mkeo unampenda, basi ishi kama mwanandoa, kubali matokeo kwamba kuna baadhi ya mambo au uhuru fulani hautaupata kama ilivyokuwa zamani ulipokuwa bachelor. Lakini huwezi kuishi maisha ya aina mbili, kwamba nusu kama mtu uliyeoa, na nusu kama mtu ambaye hajaoa - haiwezekani, na bado unataka mkeo aishi kama mwanandoa aliye mkamilifu ila wewe uishi nusu nusu. Hata kama gia yako ni kutaka kumwacha mkeo sawa, mwache lakini tambua utaacha wangapi? Halafu si umesema unampenda mkeo, sasa unamuacha kwasababu gani? Huyo mwingine una hakika gani kama hataruhusu uwe unatuma x kwa wengine?
Jifunze jinsi ya kukabiliana na hizo changamoto, hayo ndio maisha ya ndoa, unajifunza mwenzako hapendi nini una cope na maisha yanaenda, kwani wewe ni mkamilifu? hakuna vitu mwenzako anakulalamikia kama mapungufu kwako? kwa hiyo na yeye aende Jamiiforum kulalamika kama wewe? Ndoa ni kukutana na milima na mabonde, na ukishavuka, unaangalia nyuma unaona fahari kwamba nimepita kikwazo hiki kigumu. Hili likipita baada ya miezi/miaka kadhaa utajikuta siku moja unasema; "Mimi na mke wangu tumepitia wakati mgumu, tumepambana sana, na sasa tunasonga mbele.
Hasara na athari za kumuacha mkeo ni kubwa na nyingi kuliko faida tele za kubaki na mkeo na mwanao. Fikiria athari atakazopata mtoto wako na mkeo na mama yako ambaye anaelewana na mkeo. Rudi kwa mkeo muombe msamaha na kisha uendelee na maisha. Acha utoto, yakizidi omba ushauri kwa wazoefu, tutakusaidia.