Msaada tutani; Nina hali ngumu sana, nisaidieni kazi niweze kujikwamua

tembea uonemkuu...kati ya nyumba 50 nyumba 35 wenye sauti ni wanawake kwasababu uanaume wenu mnaupoteza kila siku....wanatake charge.. simameni kiume muone kama wanawake watawakalia kichwani
Ni point umezungumza kuwa “simameni kiume muone kama wanawake watawakalia kichwani”.

Nakubaliana na wewe 💯 matatizo haya yanasababishwa na sisi wenyewe wanaume. Kimaumbile mwanaume ni mtawala ila cha ajabu familia nyingi mtawala ni mwanamke, popote utapoona matoto hayana adabu hapo ujue baba kafeli ni familia inaongozwa na mama.
 
Mkuu inategema ''ntu na ntu''. Kuna wanawake jeuri hujapata kuona. Yuko tayari mzipige pale Mwenge stendi na wote nguo ziwavuke. Kwa hali kama hii unaona utaonekana kichaa, unaamua kukaa kimya.
Ni kweli unachosema, ila sema si kila mwanamke au mwanaume anafaa kwa ndoa. Tatizo linakuja pale tunapoanzisha ndoa kwa tamaa za kimwili bila kumchunguza madhaifu yake na kujiuliza kama utayamudu.
 
Tulia
 
Umeacha nyumba yako mkeo anattyombewa kiulaini.
Siku hizi wanaume ndio tunakimbia nyuma na sio wanawake tena.
Aisee kama ni kweli umezingua jombaa!!
 
Mungu akafanye njia pasipo na njia
 
cheki wababa waliozaliwa miaka ya 70kushuka nyuma...wana sauti kwa nyumba zao..kuja kuanzia 80's..hopeless...ukikomaa mwanamke anarud chini
 
usikae ndani tembea utapata mwanga..au rudi kwa tajiri yako kamuangukie
Hapa penyewe nipo ilala, na nnatembea kurudi nyumbani. Nauli 600 Sina. Mfukoni nna 200. Kuhusu tajiri yangu mbona nimeshajibu sana!? Ni mgonjwa na hayupo hapa nchini.. Km angekuwepo huyo hata hapa nisingekuja!
 
Unampaje mkeo hela yote mzee ??? Najua ni mapenzi ila mwanaume unastahili kuwa na akiba tena ya siri sana unaweka. Us8kubali kukaa kizembe na jinsia ile bro serikali upenduliwa muda wowote. Na hela ndio defence yako . Mkeo mpe kiasi tu na kisipite 30% of your income , hyo ny8ngine invest in your future.
Mwisho wanaume wacheni kuwa wawazi sana na wake zenu, namaanisha ficheni udhaifu wenu, mkeo asikuzoee sana. Mke wangu anajua nampenda ila pia anaamini nina roho mbaya yakikatili nikitaka , kama ni ufuska labda akaufanye mbeya nikiwa dar sio hapa mjini , ni muhimu uume wako ujulikane .
Ww ni baba, ngoma ya wanao na wazazi wako , ukisema kitu hata bila hasira inafaa kieleweke ndio sheria , usilete demokrasia kwa nyumba yako itapotea mazima
 
Pole sana usijiue kwa ajili ya watoto wako

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni mpumbavu.

Umetelekeza familia ukaenda kuishi na kimada ,amekuibia umekuja hapa kulia lia.

Tuanzie hapa, kipindi upo vizuri kiuchumi ulimsaidia nani? Iwe ndugu ,rafiki au mtu yeyote ?

Laana ya kutelekeza watoto imekutafuna
 
Ukakamavu pia una athari zake..! Yule tajiri angekuwepo sidhani hata hapa km ningekuja. Ni mgonjwa na hayupo hapa nchini.

Ukakamavu upi bro, acha kuwa mtu mwenye vijisababu vingi, huko ulikoikimbia familia yako kisa mke, ataingia mwanaume mwingine na kuchukua nfasi ya kujiita baba kwenye hiyo nyumba, atakua analala kwenye kitanda chako na mkeo na kuadhibu adhibu watoto wako, atakua anajifunga taulo lako na kutembea kifua wazi na kunyanyasa familia yako.
Yaani mwanaume unapaswa uilinde familia yako kwa namna yote, mimi bora nife nizikwe ila siwezi kumruhusu mwanaume aje aitawalefamilia yangu kwangu kwenye kitanda changu nikiwa hai, ayafanye baada ya kuniua.

Pambana acha vijisababu, rudi kwenye network zako, haiwezekani umefanya kazi zote hizo kusimamia biashara mbali mbali na hukuingia kwenye uhusiano na watu tofauti, changamka humo humo, wapigie simu tembeza CV yako, fight back......
 
Nikionaga mambo kama haya kwakweli hua namshukuru sana Mungu kwa kunionyesha mke anae faa.
Najiona mwenye bahati sana, sio kwa ujanja wangu bali ni kwa uwezo wa Mungu pekee.
Hakuna mtihani mgumu kama kupata mke anae faa ama mume anae faa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…