Ok niliowaona ni ndugu zangu. Walitumia mganga kwa kua wao walishindwa kunidhuru
Na nilikua mdogo sana sikua na ufahamu kwa wakati huo
Na sio wao walioniletea mganga direct bali walintumia mtu wakampa picha halisi ilivyokua kwa hiyo huyo mtu alikuja kwangu kama ananisaidia kumbe anaenda kunimalizia kabisa
Kwa hiyo ndivyo ilivyokua ila nilivyoanza kuumwa ndio niligundua nikaacha kwenda kwa huyo mganga
Ninachotafuta sasa ni tiba tuu sio kingine
Nb: usiombe uwaone wachawi watakutesa sana
Usisaha hili ni muhimu Sana sanaaaa ambalo ni sadaka sadaka sadaka sadaka......Asante
So walikuwa tayari kukuroga ili usitoe siri zao kwa mtu yoyote, lakini hapohapo wakawa tayari kumsimulia mtu mwingine picha halisi ya ilivyokuwa ili atumike kukushawishi ukubali tiba ya mganga?
Ukiwa ulikuwa ni mdogo na kwamba ulikuwa haujitambui wala kuwa na ufahamu wakati huo, ni nani aliyekusimulia?
Twende taratibu tu.
Hili ndio kosa kubwa wanalolifanya watu wengi,anaenda kwa nabii kama vile anaenda hospitali,hajui kuwa huyo nabii sio anayeponya,anayeponya pale ni Mungu,kwahiyo ili akuponye inatakiwa uhakikishe una usafi wa kiroho,sio unaenda kuombewa huku una appointment na girlfriend wako mkafanye yenu,hapo utaliwa sana pesa na manabii uchwara ambao hawakufundishi wewe kumjua Mungu bali wanakufundisha kuwa mtumwa wa kusubiri miujiza...Kuhusu kwenye maombi usiende kama unaenda Hospital au kwa sheikh.Nenda kama unaenda kukutana na aliyeuumba huo mwili unaokusmbua.Hapa na maanisha weka imani kwanza kwake.
Tatizo watu hawaamini uwepo wa covid tumia vyakula vyenye vitamin c baada ya siku nne ulete mrejesho
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Hallucinations hizo aisee
Khaa😆😆🙌🙌...wazee wa fursaVitu kutembea mwilini ni dalili ya uchawi unao mwilini mwako nitafute mimi kwa wakati wako ili niweze kukutibia upate kupona maradhi yako uguwa pole mkuu.
Aiseee pole mno, Mungu akufanyie wepesi
Sio kila mtu anaweza kuelewa, relax na pole sanaNilikua mdogo kifikra sio kiumri na mtu waliemtuma walimpa pesa kwa ni hujawahi kuona mtu anatumwa akamuue mtu
Au mtu anatumwa akamfanyie mtu mwingine ubaya kubakwa, kutekwa hata kupigwa
Why unapinga kitu nilichokishuhudia mwenywewe kwa macho yangu
Natafuta msaada kama huwezi kunisaidia Asante nashukuru watanisaidia wengine
Sio kila mtu anaweza kuelewa, relax na pole sana
Hiyo ngoma ngumu kuna kikosi kimeweka kambi kwako sheikh kaona kifo chake kipo njenje kachomoa..Lakini sheikh yuleyule mimi alikataa kunitibu sasa sijui wachawi wanawapaga rushwa
Pole sana uliyakanyagaNiliwaona wachawi wakiwa wanaenda kuloga nikawatambua ndo shida ilianzia hapo na sikuwaona mara moja
Mkuu wengine siku hizi wanafanya sijui meditation wanadanganyana huko kwenye mitandao wanafungua third eyes sasa balaa lake ndio km hili hivyo vitu ukiviamsha ujue pia kupambna sio uwe mwepesi alafu unaviamsha utaliwa mzimamzima..Mungu ndiye aliyekupa hayo macho ya kiroho, hata ukawaona. Muombe yeye Mungu huyo huyo akusaidie, akutoe kwenye taabu hiyo.
Pengine baada ya kuwaona ulichukua hatua yoyote bila kumuuliza Mungu!
Msaada wako mkubwa upo kwa Mungu wako kama ni mambo ya kishirikina yamekusababishia.