Msaada tafadhali juu ya hiki chuo.

mpenda arage

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2015
Posts
1,677
Reaction score
3,806
Habari zenu wakuu. Samahani hivi kuna mdogo wangu amenieleza kuwa, kuna chuo kinapatikana Dar es Salaam. Ambacho kinatoa kozi fupi za uhudumu wa maofisini, ambapo wanakutafutia sehemu za kufanya field, na ukishamaliza wanakutafutia sehemu ya kufanyia kazi wao wenyewe. Na ameongezea kuwa utakapopata kazi katika hizo ofisi, unao uwezo wa kupata kazi humo humo kama una ujuzi mwingine na ukaajiriwa kabisa. Kifupi yeye ana degree ya HR kwahiyo kuna mwenzie amemshawishi kusoma hizo kozi fupi. Ili wakishapata hivyo vibarua, baadae aje afanye mchakato wa kubadilikia humo humo! Kwakuwa mimi hizo taarifa ni ngeni masikioni mwangu. Ndio maana nimekuja hapa kwa wajuvi wa mambo. Isije anaenda kujipausha tu huko! Na nitafurahi zaidi kama mtanitajia na majina ya hivyo vyuo. Nitanguliza shukran zangu kwenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
Hakunaga
 

Hapa hujawa mkweli ndugu.Lazima hicho chuo kijulikane ili watu waweze kukusaidia.Utaratibu ni kwamba ndugu yako akishapata taarifa, atatafuta mawasiliano pamoja na jina la chuo.Hapo sasa tukikijua tunaweza kukusaidia.

Hivihivi tu mpaka mtu awe amekumbana nacho na bahati na wewe ukauliza.

Hata hivyo,yani hilo unahitaji msaada? Inakuingia akilini kweli zama hizi? Hiyo hata kama ni kweli mimi sijiungi na hicho chuo.
 
Nenda VETA pale hiyo kozi wanayo na ni nzuri kwa kuingilia hata utumishi then baada ya miaka mitatu anaandika barua kuelezea kama anashahada ya HR ili abadilishwe position.

Lakini baada ya kusoma VETA na kumaliza wala hawakutafutii kazi hivyo utapambana na hali yako,kwa utumishi wanatangaza sana nafasi za uhudumu mara nyingi kigezo ni cheti cha kidato cha nne,kama utakuwa umesoma hiyo kozi na vyeti unavyo itakuwa additional advantage.
 

Ulipoandika tu eti" KUNA CHUO KINAPATIKANA DSM" nimekudharau..
 
Hii habari ya chuo cha namna hii hata mimi sijaiamini. Na nikamuomba anitajie jina la chuo hicho akagoma. Na imeleta mtafaruku mkubwa, ndio maana nikakurupuka kuja kuuliza huku. Mimi mwenyewe nina ufahamu wa kutosha juu ya hizi mambo. Iwapo angenitajia wala nisingekuja huku. Ningekusanya taarifa mwenyewe mkuu. Sijamuamini kama kuna chuo cha hivyo, na yeye analazimisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Unalazimishwaje na mdogo wako wewe? .. huu uzi unauharibu kwa namna unavyo jielezea watu wanashindwa wakusaidie nini sasa
 
Mleta mada amekosa kitu kimoja kinaitwa focus
 
Mleta mada amekosa kitu kimoja kinaitwa focus
Umebishana na udogo wako ,mkashindwa kufika muafaka,ukaja kuanzisha uzi Jf.
Cha muhimu ungemtaka(siyo kumuomba) akuletee jina na mahali chuo kilipo. Baada ya kupata jina la chuo ndiyo ungekuja kuanzisha uzi apa Jf ili upate details zaidi kuhusu hicho chuo .
Pia angalia title ya uzi wako imekaa kiujanjaujanja,yaani mtu akisoma title atadhani unalo jina la chuo tayari
 
Kama mdogo wako wa kike amegoma kukutajia jina LA chuo na amekisifia kwamba kipo Dar es salaam na kama amehitimu shahada ya HR, huyo si mdogo wako Bali mkubwa mwenzio, baada ya kuhitimu na kukosa ajira ameamua kujiongeza akatafute maisha jijini, mwache aende, usibishane naye sana. Maadam chuo anakijua yeye na mahali kilipo, Hugo no MTU mzima, anajua alilolipanga kichwani make, bintj mwenye degree ya Human resource hatashindwa kujimanage maana na yeye in resource pia. Vinginevyo atatoroka nyumbani au atakuletea kichanga uleee
 
Hicho chuo kipo Mkuu, Kinaitwa Magumashi College of Home Economics (MCHE). Kipo Majohe, Dar Si Salaama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…