Msaada: Subaru Foster

Msaada: Subaru Foster

rupande

Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
47
Reaction score
5
Yeyote anayejua vizuri juu ya Magari aina ya Subaru Forester naomba anisaidie. Nataka kujua juu ya garama za spare parts, uimara wake kwa matumizi ya Barbara zetu na fuel consumption. Asante ni wadau
 
Yeyote anayejua vizuri juu ya Magari aina ya Subaru Forester naomba anisaidie. Nataka kujua juu ya garama za spare parts, uimara wake kwa matumizi ya Barbara zetu na fuel consumption. Asante ni wadau

aisee.......huku Yaeda zipo za kutosha........sijui mambo yake sana.......ila naamini magari yakiwa mengi sehemu basi mambo mswano.........mpaka kuna chama kinaitwa Subaru Kaskazini........karibu ujiunge.........
 
Watoto wa Arusha wanakuja sasa hivi kutiririka hapa, we subiri tu kidogo au unaweza pia kupitia kuna nyuzi nyingine nyingi tu kuhusu Forester. Kuna kitu kimoja mimi ninaweza kukusaidi labda wewe unapotaka gari lengo lako hasa ni nini? yaani namaanisha uimara wa gari, economical car, mvuto wa gari au nini hasa? Manake kama unazingatia uimara forester ni ngumu sana na hasa ukizipata zite za nyuma kidogo, lakini kwenye suala la unywaji wa mafuta usitegemee kabisa kwamba kwa lita moja utapata km 18 kama vitz au Swift, kuhusu mvuto hapo kila mtu na ladha yake, mimi binafsi hizi forester XT zenye turbo huwa nazipenda zaidi. Kingine hizi gari huwa zinakimbia sana na ndo maana zinapendwa na vijana wa kisasa angalau ni hatari hasa kwa barabara zetu za shilingi mia tano mia tano. Kwa hiyo akili kumkichwa, lakini vile vile vipuri vya hizi gari siyo issue tena na hata mafundi wanazidi kuongezeka kutokana na demand kuwa kubwa. Ushauri wangu nunua Subaru iliyo kwenye hali nzuri ili usije jenga urafiki na mafundi, yaani we ukienda kwa fundi labda ni kujaza upepo tairi tu na baada ya muda fulani kufanya service, ambayo hasa unatakiwa uizingatie kweli kama unapenda gari yako.
 
Back
Top Bottom