Msaada: Sielewi tofauti ya dunia na ulimwengu

Msaada: Sielewi tofauti ya dunia na ulimwengu

Dunia ni kitu kipana kidogo. Unaweza ukaiita dunia (WORLD) ukimaanisha ardhi na bahari ambavyo vinatumiwa na wanadamu katika kuigawa ndani ya mipaka ya kiutawala ya nchi mbalimbali (states, countries na nations).

Hata hivyo tafasri sahihi ya kijiografia ya neno DUNIA ni (EARTH) ambapo hapa inachukua ardhi, bahari pamoja na atmosphere. Atmosphere ni layer ya anga ya juu ya uso wa dunia yenye umbali wa wastani wa kilomita 900 na zaidi.

Hapa ndiko watu hawajawahi kuelewa vyema. Anga hiyo ina hewa za Nitrogen, Oxygen, Carbondioxide na nyingine ndogo sana. Anga hilo huwa nalo linazunguka DUNIA yetu kipindi inapokuwa inajizungusha kwenye mhimili wake (rotation) ama inapolizunguka jua (revolution).

Ndiyo maana ndege za kawaida haziwezi kuzidi anga hilo la kawaida ambalo limegawanyika na kuunda troposphere, stratosphere (na ionosphere) na exosphere. Ni warusi ndio walianza kugundua teknolojia ya kuvuka anga la dunia mwaka 1957 na kuingia anga la nje ya dunia.

Eneo hilo la nje ya Dunia ni kwa sababu haliko kwenye influence ya gravitational force ya dunia. Ukivuka anga la dunia yetu hiyo unaweza kuvutwa na kitu kingine chochote kwani eneo hilo halina gravity ya dunia.

Kwa upande wa ulimwengu ni universe yaani vitu vyote vilivyomo angani kama nyota, sayari na vimondo pamoja na vitu vingine vya kitaalam zaidi. La muhimu ni kuwa, ulimwengu ni mkubwa sana kiasi kwamba kwa kueleza tu hapa huwezi ukapata picha nzuri kwani kuna mifumo ya jua mingi, galaxies mabilioni nk, nk.
 
Dunia au earth kwa kidhungu na Ulimwengu aka World ni everything ndani yk ikijumuisha wanadamu.
 
dunia ni sayar wanayoish binadamu uliwengu ni sayar zote kuna viumbe wanaishi kwenye jua ambao kuna tetesi ndio makaz ya malaika na Allah subihanah wataaalaah na sayar zingine zote nu ulimwengu
 
dunia ipo ndani ya ulimwengu, yani sayari zote ikiwemo dunia zipo ndani ya ulimwengu, kwa hiyo binaadamu ili tuuone ulimwengu inatakiwa tuvuke dunia na matabaka yake ndo tuukute ulimwengu


~Nimejitahidi kukutoa matongo tongo mkuu
 
Dunia ni kitu kipana kidogo. Unaweza ukaiita dunia (WORLD) ukimaanisha ardhi na bahari ambavyo vinatumiwa na wanadamu katika kuigawa ndani ya mipaka ya kiutawala ya nchi mbalimbal...
Ahsante sana mlio toa majibu kwani hata mimi swali hili lilikuwa linanichanganya bt nimeelewa sasa kuwa Dunia ni tofauti na Ulimwengu.
 
Back
Top Bottom