Salaam Wana-JF Doctor!
Niende moja kwa moja kwenye mada! Mtoto wa sister yangu mwenye umri wa miaka 3 anateseka sana kwa ugonjwa ambao hapo kabla tuliamini ulitokana na kula samaki. Kwa kifupi miguuni anaota maupele makubwa, na baada ya kuhangaika huku na kule including kwenye hospitali kadhaa, tukaambiwa huo ugonjwa unaitwa Pumu ya Ngozi! Ana huu ugonjwa kwa zaidi ya mwaka sasa, ulianza kama masihara lakini hivi sasa ni kama unazidi.
Kwa maelezo hayo hapo juu, kwa yeyote mwenye lolote la kusema linaloweza kumsaidia uncle, tafadhali naomba msaada huo. Maelezo kama hospitali bora kwa hili tatizo (tumejaribu kwenye hospital kadhaa), tiba na taabibu wa asili ama chochote kile.
Natanguliza shukrani zangu kwenu.
MICHANGO YA WADAU
Niende moja kwa moja kwenye mada! Mtoto wa sister yangu mwenye umri wa miaka 3 anateseka sana kwa ugonjwa ambao hapo kabla tuliamini ulitokana na kula samaki. Kwa kifupi miguuni anaota maupele makubwa, na baada ya kuhangaika huku na kule including kwenye hospitali kadhaa, tukaambiwa huo ugonjwa unaitwa Pumu ya Ngozi! Ana huu ugonjwa kwa zaidi ya mwaka sasa, ulianza kama masihara lakini hivi sasa ni kama unazidi.
Kwa maelezo hayo hapo juu, kwa yeyote mwenye lolote la kusema linaloweza kumsaidia uncle, tafadhali naomba msaada huo. Maelezo kama hospitali bora kwa hili tatizo (tumejaribu kwenye hospital kadhaa), tiba na taabibu wa asili ama chochote kile.
Natanguliza shukrani zangu kwenu.
--------------myplusbee,
Pumu ya ngozi (Eczema)
Pumu ya ngozi au kwa kitaalamu Eczema (atopic dermatitis au atopic eczema) ni ugonjwa wa ngozi unaosababisha kuvimba kwa ngozi (inflammation). Hii huambatana na ngozi kuwasha, kuwa nyekundu, kavu, vipele na mabaka.
Maradhi haya hushambulia zaidi watoto na huweza kupitiliza mpaka ukubwani, pia lakini kwa wengi huwa yanapungua kadri mtoto anavyokua. Karibu asilimia themanini (80) ya wagonjwa wa pumu ya ngozi huanza kuugua maradhi haya wakiwa chini ya umri wa miaka mitano (5). Wagonjwa wengi pia huonyesha dalili za maradhi haya wakiwa na umri chini ya mwaka mmoja.
Aina ya pumu ya ngozi;
Dyshidrotic and Nummular dermatitis hii pumu ya ngozi huathiri vidole mikono na miguu huwa na vipele vidogo. Pia ngozi huwasha sana na hukakama huwapta sana wanawake na wanaume.
Seborrheic dermatitis hii ni pumu inayotokea pembe zoni mwa macho na pua na masikio yani usoni kwa ujumla
Dalili zake
Maradhi haya ni ya muda mrefu nikimaanisha kuwa mtu huweza kukaa nayo kwa muda mrefu, ingawa si kuwa muda wote ngozi huonyesha dalili za maradhi. Watu wenye maradhi hupitia vipindi ambavyo ngozi hututumka na kuonyesha dalili za maradhi na vipindi ambavyo ngozi huonekana kama imepona ovyo kutoonyesha dalili yoyote ya maradhi.
Dalili za pumu ya ngozi ni kama zifuatazo:
-Sehemu ya ngozi iliyoathirika huwa inakuwa kavu (inaonekana kavu),
-Sehemu ya ngozi iliyoathirika huwa inatutumuka au inavimba,
-Ngozi huwasha na kama ukikuna kwa muda mrefu basi hupasuka na kuweza kusababisha vidonda na kuleta maumivu makali.
-Ngozi huwa inakua na mipasuko inayoweza kuruhusu vimelea vya maradhi kushambulia sehemu za ndani za ngozi.
-Muwasho wa ngozi huwa mkali zaidi nyakati za usiku na joto kali,
-Maeneo yenye athari huwa yanavimba (au kututumka) na kuwa na joto.
-Maeneo ya ngozi yaliyoathirika huweza pia kuwa na malengelenge na hata kutoa majimaji.
Chanzo cha pumu ya ngozi
Uchunguzi umeonyesha kwamba kwa watu wenye ugonjwa wa Pumu ya ngozi (Eczema atopic), kuna kasoro za maumbile kwamba kusababisha upungufu wa protini fulani (kama vile filaggrin) ambayo ni muhimu katika kudumisha kizuizi ya ngozi ya kawaida. ni ambapo kinga ya mwili inapungukiwa na protini na kushambulia protini za bacteria au virus na kufanya mwili kufeli kutofautisha na kupelekea inflammation kama vile; Ukavu wa ngozi, Kukaa mazingira ya baridi sana, Mgusano wa kemikali zisizo endana na mwili, mafuta ya nywele,pafyum au vipodozi visivyo endana na ngozi yako,vyakula ambayo zina alllege na mafuta sana.
TIBA YA PUMU YA NGOZI
Crystal cell ni tiba yenye uwezo wa kufanya kazi ya kuboresha na kukarabati cell za mwili zinahusika na kuzalisha protein inasaidia kinga mwili kuhimarishwa na kuilinda ngozi.
Triple 3-miracle intense essence ni tiba ya kuondoa ngozi kuwa nyekundu, kuvimba na kupasuka. hupambana na kuondoa muwasho na kukauka kwa ngozi na kufanya ngozi iwe na muoneknao bora. Hukarabati seli za ngozi na kufanya ngozi iwe na unyevunyevu na yeneye kinga.Ni ya kupaka kwenye mwili nje.
kwa mawasiliano zaidi whatapp namba 0682315816
--------------myplusbee,
Pole sana mkuu, mie second born wangu wa kike ulimtesa toka akiwa na wiki moja! Tulizunguka kila kona kutafuta tiba lakini hatukufanikiwa, akiwa na mwaka mmoja tulikwenda nae likizo Moshi, nikiwa kwenye mizunguko na huyo mtoto kuna Mmasai alimuona akasema ninayo dawa ya hii kitu! Nikamwambia nipe akanipa kwa gharama ya shilingi 10,000 tuu!
Kwenye chupa ya dawa ya PPF, dawa ya kupaka, mafuta meusi so ukimpaka anakuwa kama kapakwa masizi na ingine ya unga ya kulamba.
Nilianza na kumpaka coz vitu ambavyo sijathibitisha ubora huwa simlishi mtoto! Huwezi kuamini, baada ya siku nne vilianza kupotea na akaanza kufurahia maisha, mwishowe vikapotea kabisaaaa!! Nikaamua na ya kulamba nimpe, mpaka leo havijarudi serious tena ila huwa vinakuja nyuma ya goti na kwenye kiungo cha mkono na kupotea!!
Sharti nililopewa ni asile parachichi, kuna siku nikampa milkshake ina parachichi ukarudi nikamtibia ukaondoka kwa hiyo hiyo dawa! Baada ya hapo nimepiga ban maparachichi nyumbani kwangu. Ugonjwa unatesa huu balaaa.
Wapare wanauita Kiguma wazungu wanauita Eczema. Actually hauna tiba za hospitali zaidi ya kemikali za kuchuna ngozi. Tiba iliyopo ni za asili kwa huku kwetu Africa
-------------Kijana wangu aliwahi patwa na hiyo hali ya vipele kwenye mikono na miguu, vilikuwa vinajirudia rudia. Na vyakula vilivyokuwa vinamuathiri vilikuwa
Samaki na Dagaa
Blue Band
Maparachichi
Pale Morocco kwa Dr. Massawe kuna jamaa anaitwa Dr. Dulla yeye alitwambia tuwe waangalifu na vyakula ila hilo tatizo halitokoma moja kwa moja mpaka mtoto avuke miaka 6. Ilifikia wakati tokana na yale mapele mpaka baadhi ya jamaa wakadhani mtoto kazaliwa na Ngoma, baada ya miaka 6 kweli tatizo limekwisha kabisa.
Kuna mafuta na Sabuni inaitwa Samona toka Uganda kwa kiasi fulani viliweza kumsaidia kijana lakini sio kumaliza tatizo
Ila hayo Mafuta na Sabuni kwa sasa hapa Dsm yamechezewa sana ni ngumu kupata Original labda kama unapata mtu anaetokea Uganda aje nayo
Mtoto wangu naye anashida kama hiyo ingawa huyo wa kwako ni chronic eczema.
Aliandikiwa dawa za allergy na mafuta ambayo ni gharama sana. Kumbuka huu ugonjwa hauponi bali unatulia ukifuata masharti na kujirudia kama hautafuata masharti. Cha kuzingatia.
1. Akioga au kunawa akaushwe na taulo safi na kavu. Usirudie kutumie taulo mpaka lifuliwe na kuukaslushwa.
2. Zingatia usafi wa nguo ns mashuka yske yasiwe na unyevunyevu viwe safi na kavu.
3. Atumie sabuni ya jamaa au B25. Kamwe asitumie sabuni nyingine zaidi ya hizi
4. Apake mafute ya mgando ya Vaseline Blue seal. Ile ambayo haina harufu wala manukato.
5. Perfume na lotion mwiko. Wala mtu au mama anayemsaidia asitumie hivi vitu.
6. Aepuke kuvalishwa nguo nyingi kila inapobidi.
7.Kila anapowashwa asijikune.
NB: Pia mcheck damu kuangalia magonjwa mengine. PITC