MSAADA: PC kuzima

MSAADA: PC kuzima

BlackWolf

Member
Joined
Aug 1, 2015
Posts
11
Reaction score
18
Habari wa weekend wanajamvi!
Naomba msaada wa kuelewa hili tatizo, nina PC hapa EliteBook HP kuanzia jana jioni inaleta maruweruwe.
Nikiwa naitumia inazima ghafla hata kama chaji iko ya kutosha na nimejaribu pia ikiwa direct connected na chaja.
Kimbembe kinakuja ikijizima, kuwaka inachukua muda kidogo na itafanya hivyo mara kadhaa kabla ya kukaa sawa na tatizo kujirudia baada ya muda.

Naomba msaada wa kitaalamu kwa wajuvi wa mambo
Asanteni!
 
Umejaribu kuchomoa hard-disk na kuirudishia? Maana kuna uwezekano ikawa imelegea...na pia na fan yake unaisikia ikiwa inazunguka na kupooza?
 
cooling system yake ina tatizo,,, unapatikana wapi??? inatakiwa kufunguliwa na kuwekwa cooling compound na fan kupigwa blower,,
 
Hiyo computer inachemka sana mkuu....
Fanya utaratibu wa kurekebisha miundombinu ya upoozeshaji wa pc tatzo linaisha
 
Yangu imezima nikapeleka kwa fundi mpka leo imezima tuu,nikaichukua,kuna siku ikawaka kisha nilipozima ndo mazimaa
 
Umejaribu kuchomoa hard-disk na kuirudishia? Maana kuna uwezekano ikawa imelegea...na pia na fan yake unaisikia ikiwa inazunguka na kupooza?
Hilo suala la hard-disk sijafanyia kazi ila nadhani fundi ananihusu hapa.
 
Hilo suala la hard-disk sijafanyia kazi ila nadhani fundi ananihusu hapa.
Ishu ya hard-disk unaweza ukalifanyia kazi labda kama ni mgeni ktk masuala ya computer, na pia unaweza ukatafuta tutorial mtandaoni ya namna ya kufungua hard-disk kutoka kwenye pc(jina & model ya pc).
....
Vipi kuhusu fan, inafanya kazi?
 
Back
Top Bottom