Juliana Shonza
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 2,009
- 1,607
Miongoni mwa mambo ya msingi sana ambayo kila mwanasiasa ama taasisi ya siasa wanatakiwa kuwa nayo ni DIRA, Dira ndio inatoa mwelekeo kwenye mpango kazi kuwa mnaamua kuwa na taasisi ya aina gani, ifikie malengo yapi na kwa muda gani. Mkikosa DIRA taasisi yenu siku zote itaendeshwa kwa mitazamo na maono ya baadhi ya watu ama mtu na atawapeleka pale anapoona yeye ni sahihi na kwa wakati anaojisikia yeye kuwapeleka hapo.
Nifupishe maandishi, nimeona kwenye vyombo vya habari leo hii, wameandika LOWASSA: NITAIJENGA CHADEMA na wameendelea kwenye story hiyo kuelezea mpango wa ziara za kichama nchi nzima ambazo EDO amejiandaa kuzifanya. Sawa..ila naomba niwasaidie kufikiri.
1. TATHIMINI.
Naomba kuwauliza, mliwahi kukutana na kupeana tathimini za matokeo ya uuchaguzi mkuu, mkaulizana wapi mliteleza na wapi mlipatia..??? ili sasa katika mpango wa KUIJENGA CHADEMA muanze na pale mlipoteleza.
Lakini swali lingine la msingi sana, Mmefanya tathimini ndani ya miezi sita ya MAGUFULI '"the bulldozer'' madarakani "HALI YA SIASA"ya nchi imekaaje..? mmeusoma upepo..?
Naomba niwasaidie TAKWIMU fupi kabisa;
a) Wananchi "hata wanachama na viongozi wa Chadema" wanaendelea kuiunga mkono Serikali ya CCM chini ya MAGUFULI. Hatua zinazoendelea kuchukuliwa za kutumbua majipu "ambazo CHADEMA kwa influence ya EDO wanazipinga" wananchi wanazikubali. Taasisi ya CZI wametoa majibu ya utafiti wao wakionyesha kuwa MAGUFULI ni namba moja the most influencial figure kwa sasa, wakifuatiwa na akina MAJALIWA na wengineo,,,LOWASSA hata kwenye 20 bora hayupo...,how could he build your party.,kwa influence gani..?
b) LOWASSA anakimbiwa na aliowaita "MARAFIKI ZAKE" hata wale maswahiba na waimba zumari waliohama nae wakitoka CCM wanarudi makundi kwa makundi, Vijana wake wa 4U Movement and Lowassa for Change ni Vinara wa kumkana kwenye mitandao, leo Peter Mwininga na kundi lake, hatawaki kabisa kuhusishwa na Lowassa, Mwapachu amesharudi, Kingunge, Mgeja na Msindai wameandika barua kwa Mwenyekiti wa CCM ili waweze kurudishwa.
Wenyeviti wa UVCCM wa Mikoa na Wilaya waliohama kipindi cha uchaguzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wilaya ya ROMBO Beatrice Condrad wamerudi CCM, makundi kwa makundi ya Vijana wanajiunga na CCM hasa wale Viongozi wa CHADEMA.
TAKWIMU Hazidanganyi, Wenyeviti wa BAVICHA wa Wilaya zaidi ya TANO wameshajiunga na CCM ndani ya Miezi sita ya utawala wa MAGUFULI tena kutoka katika Mikoa ambayo inatajwa kuwa NGOME ya CHADEMA kama yule wa MBEYA.
Wenyeviti wa CHADEMA waliojiunga na CCM nao hawana hesabu, hivi hamuangalii vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Wilaya ya Lindi Mjini na hata huyu wa Juzi tu wa Wilaya ya Iringa mjini tena Wilaya ambayo mbunge wake ni wa CHADEMA, bado uongozi wa CHAMA unateteleka..? Hamjiulizi..??
Waliokuwa wagombea UBUNGE nao wanahama CHADEMA bila hesabu, jana pekee wamerudi wawili aliyekuwa Mgombea wa Ubunge Manispaa ya Morogoro na yule wa Mvomero..bado mnasema LOWASSA is right person kukijenga CHADEMA na kwamba he's influencial enough.???
Nasema hivi, Hata Influence ndani ya MONDULI nyumbani kwake imekwisha kabisa. Kijana ambaye alikuwa Mkoba wake, mtunza siri wa nyumbani na MUUMINI wa LOWASSA Ndugu Elisante KIMARO nae AMESHAMKANA mara tatu kwenye mikutano ya hadhara ndani ya Wilaya ya MONDULI.....i can't see how is this person anakuwa MJENZI wa chama..?
Hivi mnafahamu maana ya KUJENGA chama..? neno Kujenga ama MJENZI mnafahamu ni mtu wa aina gani..???
Bado nashindwa kuelewa kuwa kimewakuta kipi ninyi ndugu zangu..? yale maarifa ya zamani yamekwenda wapi..? MJENZI wa Chama ataanza kuzunguka kwenye mikutano ya hadhara, wananchi watamuhoji juu ya kesi ya Mwanae SIOI ya WIZI wa Trilioni moja..mnataka ajibu nini..? mnajenga CHAMA gani..??? HOVYO KABISA..