Msaada: Nitapambana vipi na Mchawi?

Bila ya wewe ku define ajabu inawezekana tusielewane kwa kuwa tunaongelea vitu viwili tofauti.

Naomba unipe link ya hapo nilipopinga kuwepo maajabu nione nimepinga vipi kwa maneno yangu mwenyewe.

Mada ili inahusu "Dunia na maajabu yake"

https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/756250-dunia-na-maajabu-yake-4.html
 
Biblia yasema "HAPANA UCHAWI WALA UGANGA JUU YA ISRAELI.
[HESABU 23:23]
Una damu ya Yesu ya kumshinda mchawi (Shetani) ?
 
Biblia yasema "HAPANA UCHAWI WALA UGANGA JUU YA ISRAELI.
[HESABU 23:23]
Una damu ya Yesu ya kumshinda mchawi (Shetani) ?
Amen Mtumishi. Dawa ya hao ni Yesu Kristo.

WAPIGE KWA MOTO WA JINA LA YESU KRISTO MASHETANI WOTE WANAOHARIBU MAWAZO, Omba maombi haya.

Kwa mamlaka ya Jina la YESU KRISTO mwana wa MUNGU aliye hai ninawashia moto mashetani wote mnaoniletea mawazo mabaya kwenye akili yangu, mnaopindisha mawazo yangu ambayo MUNGU ameniwekea kwa jina la YESU KRISTO . Ninawasha moto kwa mashetani yote yanayonijia kupindisha njia zangu kwa damu ya mwana kondoo, kuanzia leo mimi sio maskini kwa jina la YESU KRISTO. Imeandikwa; "mwana wa MUNGU alidhihiriswa ili azivunjee kazi za ibilisi kuzimu," Ninazivunjavunja kazi zote za kuzimu kwa jina la YESU KRISTO, mnaopindisha mawazo ya maendeleo yangu ninawafyeka kwa upanga wa KRISTO. Katika jina la YESU enyi jeshi la mashetani mliotumwa kuja kuniletea matatizo kwenye maisha yangu ninawatetekeza kwa moto wa MUNGU aliye hai.

Imeandikwa, "neno la MUNGU ni moto ulao." Ninawateketeza mashetani wote mliotumwa na waganga wa kienyeji, wachawi mmetokea kuzimu ninawateketeza kwa moto wa Mungu kwa jina la YESU KRISTO.

Asante BWANA YESU kwa kunipa ushindi mkuu.

Ni katika jina la MUNGU BABA, MUNGU MWANA na MUNGU ROHO MTAKATIFU nimeomba. Amen.
 
MWITE SHUJAA WA MSALABA YESU KRISTO KWA MAOMBI HAYA NA UTASHINDA

Tunawafuata adui zetu palepale walipo, tunawatokea kwenye ulimwengu wa Roho na kuwakanyaga na kuwanyanganya mali zetu na vitu vyetu vyote kwa nguvu ya msalaba wa YESU KRISTO . Kwa jina la YESU nimepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui kwa jina la YESU. Kwa nguvu ya msalaba ninawafuata wachawi, waganga wa kienyeji na adui zangu wote katika ulimwengu wa roho waliokaa kikao kinyume na mimi, ninawaponda vichwa kwa jina la YESU KRISTO. Imeandikwa wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo, ninawashinda kwa damu ya YESU KRISTO.

Ninazikanyaga mamlaka zote za giza kwa damu ya mwanakondoo. Kwa nguvu ya msalaba, kwa damu ya mwanakondoo ninawashambulia wote mnaotumia baraka yangu, ninauponda uzao wa joka katika jina la YESU KRISTO. Ninawashambulia mashetani katikati ya uzao wa wanadamu kwa jina la ESU. Kwa damu ya mwanakondoo, ninavifuatilia vipawa vyangu vilivyofichwa katika mashimo kwa jina la YESU.

Ninaitumia nguvu ya msalaba kwa jina la YESU KRISTO, waliofichwa kwenye mashimo, kwenye mapori, baharini, kwenye mwezi, kwenye, kwenye anga ninawarudisha kwa damu ya YESU KRISTO. Kwa jina la YESU KRISTO ninaamuru warudishwe, natumia nguvu ya msalaba kwa damu ya YESU KRISTO, biashara zilizofungwa, kazi zilizofungwa ninazifungua kwa jina la YESU KRISTO. Nakwenda msalabani, msalaba wa furaha, msalaba wa ukombozi, msalaba wa ushindi, msalaba wa nguvu, msalaba wa maarifa nakata rufaa hapo kwa jina la YESU KRISTO.

Asante BWANA YESU kwa ajili ya kunifia msalabani, asante kwa ajili ya nguvu iliyomo ndani ya msalaba. Asante kwa ukombozi, uponyaji na msamaha wako.

Ni katika jina la YESU KRISTO nimeomba .
Amen.
 
Dawa ni Yesu Kristo Wa Nazareth aliye hai...

Yesu aliyemfufua Lazaro na ambaye kuzimu na mizimu ilitetemeka kwaajili yake....

Mwite Yesu atakusaidia....

CC: Eiyer Ntuzu Mkuu wa chuo

Ni kweli mkuu hakuna kama Yesu Kristo, kuna sala moja mkuu Telefunken amemuelekeza jinsi ya kuvunjilia mbali nguvu za giza... Damu ya Yesu hakuna inachoshindwa...
 
Last edited by a moderator:
Amina.. nimebarikiwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…