Msaada: Nina tatizo la uvimbe kwenye mfereji wa haja kubwa

ngorombo

Member
Jun 7, 2019
60
200
Habari Wana jamvi naombeni msaada wenu, nina tatizo la uvimbe kwenye Mfereji wa haja kubwa ( Mlangoni kabisa).

Nimevumilia maumivu yamezidi kuwa makali; wakati wa kukaa, kutembea na mbaya zaidi nikiwa toilet kwa short call na long call.

Kilianza kiupele kidogo ambacho maumivu yalikuwa sio makali hivyo na sikutilia maanani

Nitumie dawa gani niweze kupona au tatizo litakuwa ni nini?

Naombeni msaada wenu.
 
Mara nyingi sehemu kama hizi kila Mtu atatoa Dawa yake au ushauri wake ili akusaidie, lakini wengi watakupa huo ushauri na hatimae hujui ufate wa nani au uuache wa nani..... hiyo ni Afya Ndugu yangu, wahi kwa Hospital mapema
 
Uvimbe kwenye mfereji wa haja kubwa?

Sema una uvimbe mkunduni! Mfereji ndio nini!

Hivi hivi utakosa tiba kwa kujifanya unatunza Kiswahili!

Kama mkundu una uvimbe sema mkundu wangu una uvimbe! Sio mambo ya mifereji, sijui mfereji wa haja kubwa!

Anyway, pole.
 
Bawasiri hiyo tafta alovera, mlonge, mnyonyo na kitunguu saum changanya vyote kwa pamoja uwe unapaka kila unapotoka kujisaidia haja kubwa!

Dozi ya pili chukua parachichi, tangawizi, chaza, mzeituni na mbegu za papai changanya huo mchanganyiko wote na asali unywe asubuhi kabla ya kula au kunywa kitu chochote!
 
Bawasiri nafikiri hiyo! Ufumbuzi upo humuhumu nilishawahi soma humu mgagani ndo tiba search kwenye jf search upate maelezo namna ya kuuandaa..

Ushauri wangu ukipona uwe na mtindo wa kufanya mazoezi pili usikae sana walau uwe unafanya matembezi.

Kama unakilo nyingi punguza ziendane na umri na kimo chako pia zingatia mlo mzuri,maji kwa wingi usisahau mboga za majani pia ona ni kufuru kupata choo kigumu laiti ukizingatia hayo hata choo chako kitalainika!.

Ugua pole.
 
Uvimbe kwenye mfereji wa haja kubwa?

Sema una uvimbe mkunduni! Mfereji ndio nini!

Hivi hivi utakosa tiba kwa kujifanya unatunza Kiswahili!

Kama mkundu una uvimbe sema mkundu wangu una uvimbe! Sio mambo ya mifereji, sijui mfereji wa haja kubwa!

Anyway, pole.
Anaupoza ugonjwa...wakat tatizo ni kubwaa...USICHEZE NA SEHEMU ZA SIRI.....
 
Tiba ya kiasili hio ya bawasiri vp inakusumbua nikupe dozi nyepesi!
Nimeuliza ukinipata nijue jinsi ya kufanya au mtu akilalamika nimwambie tiba ndugu. Kumbe kuna dozi nyepesi?.basi hayo ni magumashi
 
Habari Wana jamvi naombeni msaada wenu, nina tatizo la uvimbe kwenye Mfereji wa haja kubwa ( Mlangoni kabisa).

Nimevumilia maumivu yamezidi kuwa makali; wakati wa kukaa, kutembea na mbaya zaidi nikiwa toilet kwa short call na long call.

Kilianza kiupele kidogo ambacho maumivu yalikuwa sio makali hivyo na sikutilia maanani

Nitumie dawa gani niweze kupona au tatizo litakuwa ni nini?

Naombeni msaada wenu.
iponde tangawizi mbichi maji maji yake pakaa hapo kwenye uvimbe asbui na jioni for within 1 week utakua umeshapona ila utavulia maumivu kdogo
 
Nimeuliza ukinipata nijue jinsi ya kufanya au mtu akilalamika nimwambie tiba ndugu. Kumbe kuna dozi nyepesi?.basi hayo ni magumashi
Ndio dozi nyepesi ipo ni cream inauzwa dukani!
 
Habari Wana jamvi naombeni msaada wenu, nina tatizo la uvimbe kwenye Mfereji wa haja kubwa ( Mlangoni kabisa).

Nimevumilia maumivu yamezidi kuwa makali; wakati wa kukaa, kutembea na mbaya zaidi nikiwa toilet kwa short call na long call.

Kilianza kiupele kidogo ambacho maumivu yalikuwa sio makali hivyo na sikutilia maanani

Nitumie dawa gani niweze kupona au tatizo litakuwa ni nini?

Naombeni msaada wenu.
Dawa ni hii AloeTFCG

inaweza kusaidia, kuponya, kutibu au kuzuia ...

Kuuma Misuli

Ugonjwa wa Asidi Reflux (Reflux Acid)

Ugonjwa wa Arthritis

Pumu

Fizi za Kutokwa na damu

Majipu

Ugonjwa wa utumbo

Saratani

Cholesterol

Ugonjwa wa Uchovu wa muda mrefu

Kuvimbiwa

COPD

Ugonjwa wa Crohns

Ugonjwa wa ngozi

Kisukari

Diverticulum

Eczema

Fibromyalgia

Malengelenge sehemu za siri

Gout

Homa ya nyasi

Bawasiri na Rundo la Kutokwa na Damu

VVU

Shughuli ya kuzuia virusi na uvimbe: Vitendo hivi vinaweza kutokana na athari zisizo za moja kwa moja au za moja kwa moja. Athari ya moja kwa moja ni kutokana na kusisimua kwa mfumo wa kinga na athari ya moja kwa moja ni kutokana na anthraquinones. .anthraquinone aloin huzima virusi mbalimbali vilivyofunikwa kama vile herpes simplex, varisela zosta na influenza.

Shinikizo la damu

Cystitis

Ugonjwa wa Utumbo unaowaka (IBS)

Maumivu ya Viungo

Mawe kwenyeFigo

Ini

Lupus

Malaria

Migraine
.Milia

Pancreatitis

Psoriasis

Ugonjwa wa Rhematism

Scalds

Matatizo ya Sinus

Athari za Ngozi kutoka kwa Tiba ya Mionzi

Tendinitis

Neuralgia ya Trigeminal

Colitis ya Vidonda

Vidonda vya Mdomo

Vidonda vya Ngozi

Vidonda vya Tumbo

Mshipa wa Varicose

Inaweza kusaidia mifupa yako kuwa na afya kadri umri unavyosonga

Husaidia misuli yako kufanya kazi vizuri

Afya ya usagaji chakula

Bidhaa hii ina virutubisho kama vitamin 12 ikiwemo B12, madini 20 , amino acid 18 na enzymes.

.
 
Back
Top Bottom