publito
JF-Expert Member
- Nov 13, 2016
- 551
- 617
Wakuu amani kwenu,
Takribani wiki chache zilizopita niliibiwa simu na mazingira ya kuibiwa yalikuwa hivi; Mimi nina stationary maeneo ya vingunguti, sasa mashine yangu ya printer ilikuwa inasumbua hivyo ikabidi nimpigie rafiki yangu mmoja ambaye naye anayo stationary ili aweze kunielekeza fundi wa printer.
Na kweli baada ya siku chache alimuelekeza fundi ambaye huwa anamrekebishia mashine yake, huyo fundi alikuja siku ya kwanza akaitengeneza lakini akawa hajamaliza, hivyo ikabidi harudi siku ya pili kwa ajili ya kumalizia.
Sasa siku ya pili aliyorudi kwa ajili ya kumaliza alikaa muda mrefu kidogo na baadae akawa ameniomba maji ya kunywa, kitendo cha kwenda kumchukulia maji kama dakika mbili tu nikakuta kashakimbia na baadhi ya vitu ikiwemo na simu kubwa.
Lakini kwa kuwa tayari nilikuwa na mawasiliano yake pamoja na yule mtu ambaye alimuelekeza kwangu nikawa na matumaini pengine naweza kumpata, lakini muda mchache baadae yule mwizi akawa anatumia laini zangu zile kwa ajili ya kuombea pesa kwa njia ya sms akijifanya ni mimi,
Hivyo ikabidi nipige simu tigo na airtel kwa ajili ya kufunga laini hizo, kesho yake ikabidi niende kutoa taarifa polisi na nimepewa RB, lakini mpaka sasa namba ya huyo mwizi mpaka sasa inapatikana na jina lake ukilingalia tigo pesa linakuja hilo hilo jina lake ambalo analitumia,
Nilijaribu kuwapigia tigo kuwaomba msaada kama wanaweza kunipa details za huyo mtu kwa kuwa tayari nina RB lakini wamesema wao hawawezi kutoa taarifa za mtu yeyote.
Katika kuomba ushauri kuna mdau mmoja aliniambia kuwa unaweza kumtrack mtu kwa kutumia namba ya simu, nilivyomfuata yule mtu ambaye alimuelekeza kwangu akaniambia kuwa hata yeye alikuwa anamtengenezea lakini hajui wapi anaishi.
Picha yake ninayo na namba yake ninayo hivyo humu kama mtaalamu wa IT au kuna mtu ambaye anaweza kunisaidia kwa njia yoyote ile hata kwa ushauri naomba anisaidie maana kwa kipindi hiki kanirudisha sana nyuma.
NATANGULIZA SHUKRANI KWENU.