Habarini?
Mi ni mwanajf wa kuperuzi kama guest. Lakini leo nimepatwa na nimelazimika kupata ac ili mnisaidie kwa ushauri.
Ipo hivi, mimi nilikua na mpenzi ambaye huu ni mwaka wa tatu sasa. Miaka miwili nyuma ilikuwa ni furaha na pia alikuwa akitaka hata aje kujitambulisha rasmi. Nyumbani walimjua na aliweza kuja muda wowote hata kama sipo nami pia nilijulikana kwao hata kama hayupo niliweza kwenda. Kiufupi kila mmoja alikuwa free na comfortable.
Shida imeanza mwaka wa tatu wa mapenzi yetu. Mwenzangu mapenzi yalishuka. Kupiga simu ilikuwa shida. Nikimpigia yu busy. Kila siku alikua ananiletea visa. Hata pasipo na kosa ye alilitafuta kosa lilipo akalipachika. Nakumbuka kipindi hiko nililia sana. Nilisali sana. Lakini mambo hayakubadilika. Mwisho wa siku mwenzangu akaniambia kuwa amepata replacement yangu hivyo hanihitaji katika maisha yake.
Tatizo linalojitokeza ni moja. Kiukweli mi nampenda sana. Ye ni kama ndugu yangu mbali na mpenzi tulikuwa kama marafiki na ndugu. Shida zake zangu na zangu ni zake. Tumeshajaribu kufanya projects mbalimbali.
Baada ya vituko vyote alivyonifanyia, nikamwambia mwenzangu yeye ni kama ndugu yangu. Maswala ya projects zetu zisikatike sababu ya mapenzi. Mi nimeshachoka kuhangaikia mapenzi hivyo tuendeleze kazi za kimaendeleo tu. Hata akitaka kuoa mi roho yangu ni nyeupe kabisa. Taratibu nitamuona ni mtu wa kawaida. Ila shida mwenzangu aliongea na baadhi ya watu kuwa hata iweje hawezi kuniacha. Ataenda kote lakini atarudi tu kwangu. Na pia mimi ninamtreat kama mtu wa kawaida kwa sasa lakini yeye bado ananitreat kama mpenzi. Hataki kabisa tushirikiane kimaendeleo zaidi. Kila anapojaribu kunisogelea bado anataka tuendeleze mapenzi. Anajilazimisha kujiweka mbali na mimi kwa nguvu sana jambo ambalo linamuathiri. Baada ya muda kidogo ananiomba msamaha sana
Ndugu zangu nipeni ushauri. Haiwezekani kabisa mimi kuwa na huyu mtu kwa ajili ya kazi tu?
Naombeni mnishauri ndugu zangu ili nipate kurekebisha hili tatizo. Sitaki chuki iwepo kati yetu. Kama upendo umeisha basi ibaki tu maisha ya kawaida maana kwao na kwetu wamekuwa family friend sasa. Lolote likitokea tunajumuika sote.