Msaada ndugu zangu wa JF.

Sijui kama itasaidia kupata estimates za gharama! Kuna rafiki yetu maiti yake ilisafirishwa toka CA marekani kwa total gharama ya $13,000/ hii ikiwa usafiri $6700, casket $2100 na gharama za funeral home $4200

So kwa UK l think ukiandaa kama $10,000 utamleta! I am sure wanaojua watakusaidia!
 
Pole sana uporoto01! Nakutakia ufanikiwe kuurudisha mwili wa dada yetu!
 

Dada zetu! sisi wabantu tunaweza tukawa atueleweki lakini ni watu wa imani sana aiwezi tokea mtu utelelekeze mwili wa mpenzi wako jamani sisters zangu mleni kitu hapo!je huyo ni binadam kweli?
 
Asante mkuu finally some figures.
 
Mungu akusaidia kufanikisha uletwaji wa mwili wa dada yetu. Mtu kuzikwa kwao ni jambo zuri kuliko kuishia kuwa-cremated baada ya mwili kutelekezwa.
Again, poleni sana
 
umejua kifo kimetokana na nini Uporoto? usije kuta kauawa? manake hawachelewi hawa watu....kuua si ishu kivile!!
Na kweli hili ni fundisho.....:caked:
Kwakuwa kuna postmortem ilifanywa na kuna coroner report hayo tutafatilia baadae cha muhimu kuupumzisha mwili kwenye kaburi.
 

Pole sana kamanda!mimi sijui sana ngoja tuwasubiri wenye kujua!
 
Wabongo mlioko UK, na staff wa ubalozini jamani si mumpe Uporoto details zote zinazohitajika kuhusu kusafirisha mwili?
Nawasilisha
 
pole sana uprotto zingatia shauri ulizopewa na waliotangulia kuchangia hapo juu na usisahau kufuatilia medical report cause of death.
 
Nina imani utafanikiwa, kwa kuwa kesi ni kujua figures na umesema pesa si tatizo. Mwili ukifika Dar usisahau kututaarifu hata tuje kuomboleza na wewe... All in All, POLE SANA KAKA KWA MSIBA+KERO ALIYOKULETEA MZUNGU!
 
.........pole sana, huyo mzungu ni choka mbaya na ana roho mbaya. Inakuwaje aache solemba mwili wa mkewe namna hiyo? Alimpenda akiwa mzima leo kaona maiti anaamua kumfanyia hivyo mwenzie. Fuata ushauri wa Kaunga naona kashauri vizuri.
 
Mmmh, hii kali ya mwaka. Kwanza pole sana kwa yaliyokukuta.

How come mume wa ndoa aitelekeze maiti ya mkewe halafu serikali inakaa kimya? Inawezekana ukautoa huo mwili, wewe lipa gharama za usafiri tuwakumleta bongo, gharama za kukaa kwenye friji hizo wiki mbili alipe huyo mume wake.
 
Pole sana Uporoto. I hope utapata msaada soon. Kila la kheri katika hili.


Kha...ivi kweli wewe umesoma? Sidhani mtu aliyesoma anaweza kuandika namna hii. Huwezi kusema rangi ya mtu inachangia character ya mtu. Rangi ya ngozi ni 1/6 of an inch. Na sijasoma hata siku kuwa rangi inachangia mawazo na utendaji wa mtu. Ni aibu kwa wewe kuandika huu ujinga hapa. Umetumia incidents chache ku-generalise. Tatizo nililoona mimi ni kwamba wazungu wana character moja ya kujiona! na kuona kila mwaafrika anawataka wao tu. Na hilo limetokana na tabia za wa kaka na dada wengi wa kiafrika! Bila sisi kubadilisha hizi tabia tutaendelea kuonekana mafala, omba omba, watu wanaojipendekeza.
Nahofia sana pale unaposema kuwa rangi ya mtu ina maana ni mtu wa namna fulani. Hapo umekosea na unavuka mpaka.
 
Pole sana uporoto01 kwa msiba mkubwa uliokufika. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN.
 

Cheki na wizara ya mambo ya nje watakuwa wanazifahamu gharama hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…