Msaada natafuta kazi

Msaada natafuta kazi

Flamegood

Senior Member
Joined
Oct 27, 2018
Posts
129
Reaction score
293
Habari wana JF,

Kama head inavyosema hapo juu,

Mimi ni kijana Wa miaka 20 naishi Dar es Salaam, Nina elimu ya kidato cha nne, nilimaliza mwaka 2017 Arusha, ufaulu wangu haukua mzuri kwa kuwa nilipata Daraja la nne, Kutokana na hali duni ya kimaisha wazazi walishindwa kuniendeleza na Chuo, Hivyo nilipomaliza masomo hayo ilibidi nije Dar kwa Mjomba ambae aliahidi kuniendeleza kwenye elimu ya ufundi(mechanical)....

Lakini baada ya kuja huku hakutimiza hilo bali niliishia kufanya kazi katika viwanda vya wachina kwa miaka miwili nikagundua ile kazi haina maslahi nikaamua kuachana nayo na kuanza biashara zangu mbalimbali....Ila kwa sasa naona biashara haziniendei vizuri kwa kuwa nashinda kutengeneza japo 100k per month.......

Hivyo kutokana na hili nikapata wazo kabla ya kugive up na kurudi Mkoani nijaribu kutafuta ajira kama kuna mtu Ana connection yoyote naomba masaada....Ahsanteni
 
Endelea tu kukomaa na biashara zako mkuu maana kwa haraka haraka nilivyokusoma hauna "mentality na discipline" ya kuajiriwa...maana hata Kama mjomba wako angetimiza ahadi yake si bado ungekua fundi makenika tu ambayo ni kazi ya kujiajiri??

Biashara inahitaji muda ili ikue na kuanza kukupa faida kubwa... it's not an overnight process mkuu, usikate tamaa.

Na kwa Elimu yako hio mkuu (japo sikukatishi tamaa) ni vigumu sana kupata ajira ya kukuingizia hata hiyo laki moja kwa mwezi unayoitamani
 
Umenena ukweli.
 
Huko kwenye viwanda vya wachina ni wapi unipe connection nikatafute mtaji nijiajiri na mie.
 
Back
Top Bottom