Msaada: Naona ufafanuzi napoweza kusoma kozi ya Wildlife Menagement

Jiwe kuu01

JF-Expert Member
Jul 30, 2020
228
86
Pole na majukum wakuu,

Nimemaliza kidato cha sita Mwaka huu nataman sana kusoma Kozi ya wildlife management. Je ni chuo gan kitanifaa kwa Kozi hiyo.

Natanguliza shukran zangu za dhati Ma GT
 
Naipenda SUA lakini nafikiri Mweka imekaa vizuri zaidi wana ujuzi wa siku nyingi zaidi ya SUA.
 
SUA kua chuo kikuu haina maana wako vizuri zaidi ya vyuo vingine vya kati kwenye kila jambo.
Ni kweli lakini kuwa sua na mweka wa sua value Ni kubwa kuliko mweka. Kwa sababu hio hio ya sua kua chuo kikuu.
 
Ni kweli lakini kuwa sua na mweka wa sua value Ni kubwa kuliko mweka. Kwa sababu hio hio ya sua kua chuo kikuu.
Kinacho matter ni program ina mazoezi yanayotakiwa. Naamini Mweka watakuwa wazuri zaidi, najua practical nyingi za SUA ni wakati wa Break/Field attachment na sidhani wana muda wa kutosha ukilinganisha na mweka. Kumbuka Mweka iko chini ya wizara hivyo sidhani kama wataivale SUA zaidi ya Chuo Chao.
 
Ni kweli lakini kuwa sua na mweka wa sua value Ni kubwa kuliko mweka. Kwa sababu hio hio ya sua kua chuo kikuu.
Mkuu 'value' inategemea na kozi husika sio issue ya chuo tu. Mfano tangu huko nyuma vyuo vya IFM, TIA/DSA na IAA vimekuwa vikizalisha wahasibu/wakaguzi wazuri sana na hata mkiomba naye ajira mahali wewe ukiwa unatokea university bado hao watu toka vyuo hivyo watapewa consideration ya juu zaidi yako.

Pia vyuo kama DIT na IAA vinazalisha watu wazuri sana wa IT/Computer Science kuliko vyuo vingi vyenye majina makubwa.

Kwa maoni yangu, kwa kuwa umeomba ushauri jaribu kuzingatia ushauri utakao kujenga kiueledi. Pia bado utapata nafasi ya kushow case uwezo wako through interviews mbele ya hao wa vyuo vikuu.

Hayo mambo ya kile ni chuo kikuu huwa yapo huko level za sekondari (nayaitaga sifa za kijinga), mtu anasoma chuo chenye jina kubwa then kichwani hana kitu, jina la chuo halitakusaidia.
 
Mkuu 'value' inategemea na kozi husika sio issue ya chuo tu. Mfano tangu huko nyuma vyuo vya IFM, TIA/DSA na IAA vimekuwa vikizalisha wahasibu/wakaguzi wazuri sana na hata mkiomba naye ajira mahali wewe ukiwa unatokea university bado hao watu toka vyuo hivyo watapewa consideration ya juu zaidi yako...
Ni kweli kabisa ulivyosema mkuu inategemea na kozi husika inavyotolewa na chuo husika. Natetea sua Kama chuo kinachohusika na kozi alioulizia mleta mada.
Sua kimebaki kua chuo kikuu bora katika fani kitoazo za kilimo na wanyama.

Wao sua wako vizuri kuliko udsm ama udom nk ila wao wako specialize kwenye kilimo na wanyama. So mhitimu was sua katika fani yake huwezi kumlinganisha na mhitimu wa udom katika fani yoyote.

Kwa maana hio mweka na liti wako juu ya sua?
 
Ni kweli kabisa ulivyosema mkuu inategemea na kozi husika inavyotolewa na chuo husika.
Natetea sua Kama chuo kinachohusika na kozi alioulizia mleta mada...
Nadhani unachanganya wanyama/ufugaji na wanyama pori.

Kwa kozi za Wildlife (wanyama pori) SUA sio tu anasubiri bali anasubiri mbali kwa Mweka, na mtoa mada anataka kusoma Wildlife Management.
 
Mkuu mweka ni chuo kizuri sana hasa kwa koz ya wanyamapori, lakini changamoto yake ni ada yake na michango ipo juu mno, kozi ya wildlife kwa Sua ni 1,262,000/=TSh lakini mweka inafika 4,675,000/=Tsh kwa mwaka iyo ni school fee pekeyake na hapo bado gharama nyingine za hostel na direct cost. Niliwasiliana na muhasibu wa pale mweka nikamuuliza ikiwa mwanafunz atapewa asilimia mia ya mkopo je atalipiwa ada yote !!? Akasema ukipewa asilimia mia kwa mweka wanakulipia 1,820,000/=Tsh na nyingine iliyonaki unalipia wewe, chaguo ni lako mtoa maada kama kiuchumi mpo vizuri nakushauri uende mweka ila vinginevyo sua inakuhusu
 
Pole na majukum wakuu,

Nimemaliza kidato cha sita Mwaka huu nataman sana kusoma Kozi ya wildlife management. Je ni chuo gan kitanifaa kwa Kozi hiyo.

Natanguliza shukran zangu za dhati Ma GT
Kuna Sua na Mweka

Mweka ada yao ipo juu sana Sua ada yao ni ndogo.
Mweka wana practical nyingi kuliko Sua

Pia udsm kuna course inaitwa Bsc in wildlife science and conservation inaweza ikakufaa
 
Kama unasoma kwa ajili ya kupata ajira anzia Pasiansi update kwanza certificate baada ya hapo ndio ukasome kama ni SUA au Mweka kutokana na ada yako ila Mweka wako vizuri zaidi...
 
Back
Top Bottom