Msaada: Naomba kujulishwa mipaka ya kulipia car parking Dsm

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,422
1,791
Wana JF;

Naomba msaada kwa wanaoelewa, kuna utaratibu katika jiji la DSM na hata mikoani kuhusu kutoza ushuru wa maegesho ya magari. Na hii imekuwa ni kwa miaka mingi Manispaa zinakusanya ushuru wa maegesho sehemu mbalimbali mijini yaani jambo la kawaida. Na maeneo haya mengi ni yale ambayo manispaa husika huwa wanafanya usafi (kuna wafanyakazi wa kufagia maeneo) hivyo moja ya matumizi ya pesaile ni kulipa posho / mishahara na pia ni mapato ya manispaa.

Lakini kumekuwa na tabia sasa iimezuka pembezoni mwa jiji la DSM hasa maeneo ya viwandani; unakuta mwenye kiwanda ametengeneza kwa kuweka zege pembeni nje ya ukuta wake. Na wanakuja watu wa kutozaushuru wa maegesho na kuweka kijiwe pale kuanza kubandika makaratai ya ushuru.

Maeneo hayo hawafanyi usafi kwani wafanyakazi wakiwanda ndio wanasafisha na pia hawaja itengeneza hiyo parking.

Najiuliza je, ndilo tamko au sheria imepitishwa na manispaa kukusanya maeneo nje ya mji????

Hofu yangu isiwe ni mradi wa mtu mjanja katika hili, maana kwa kipindi hiki kila mtu anafikiria atoke vipi baada ya mianya kufungwa. huenda ni jipu hili.

Nililishuhudia jana kule Kigamboni Inidustrial Area, Vijibweni DSM.

NAOMBA MSAADA ILI SIKU NYINGINE NIKIENDA NIJIANDAE KUWA NA PESA YA USHURU.
 
Mkuu, ardhi ni mali ya serikali, ikiwa ni nje ya kiwanda na ni akiba ya barabara lazima ulipe ushuru
 
Ukija Dar jipange. Mbezi kwa msuguri parking inalipiwa Kama mujini
 
Waende wakafanye na usafi pia kama ilivyo mjini huku, maana lile eneo kipindi cha nyuma kulikuwa na majani nahakuna hata baiskeli iliyokuwa inaegesha pale,. Lakini baada ya kiwanda kuboresha nao ndio wakaona panafaa kuwa kitega uchumi. Na kama ni hifadhi ya barabara hawaoni kuwa kama ni kosa pia kuhalarisha maegesho nao wanachukua ushuru.

Nina mashaka ni mradi wa mtu huko manispaa. Kwani mwenye kiwanda alijenga kwa ajili ya wageni wanaokuja kiwandani na wafanyakazi wake wenye magari waweze kuegesha hadi jioni muda wakaazi unapomalizika.
 
mi hawa watu hata huwa siwaelewi... ushuru unatozwa kila mahala.. mara kila mtu na bei yake.. hata ukipaki mbele ya duka unaloenda wao wanadai tuu wkt wenyewe wanaruhusu
 
ningekuwa mwenye kiwanda ningepitisha greda nikapanda maua na miti tuone watatoza ushuru nyuki na vipepeo
 
Back
Top Bottom