Msaada: Nani ni tatizo ndani ya CCM?

Msaada: Nani ni tatizo ndani ya CCM?

Chama chetu cha Mapinduzi sasa hakipendwi kama mwanzo wake. Hakiaminiwi kirahisi hata pale kulikokuwa na ngome za chama chetu kama Lindi na Mtwara.Kinalalamikiwa;kinazidi kuchukiwa. Yawezekana kuna tatizo la ki-mfumo...mazoea. Lakini,wapo watu ndani ya chama chetu ambao ndio walezi wa mfumo huo unaosawajisha heshima ya chama chetu. Mkiwa kama watanzania wenye vyama na msio na vyama,ni nani hasa ni tatizo katika CCM yetu? Kwanini? Tusaidieni ili tujirekebishe na kuimarisha chama chetu. Karibuni waungwana! Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.

Mada nzuri. Tatizo la chama chetu ni pale tuliporuhusu wenye fedha kutumia fedha zao ku-influence maamuzi ndani ya chama, na pia kuruhusu utumishi ndani ya siasa kuwa biashara. Leo CCM si chama cha wananchi wa hali ya chini bali kundi la watu wenye mali tena ma-billion. Cha ajabu hata wanaoingia kwenye madaraka kupitia CCM wakiwa maskini baada ya muda wanakuwa matajiri. Hii ndiyo CCM yetu ya leo. Kuwa waziri au naibu waziri ndani ya serikali ya CCM ni kama kuokota jiwe la dhahabu.
 
524013_586478848062505_1523896972_n.jpg
 
CCM ni kama kansa kwenye ini ambayo ni mpaka ufanye transplant....ndo mtu anakuwa mzima la sivyo ukiondoa kipande kidogo...unamuongezea mtu miezi 6 tu ya kuishi na kufa....so transplant ya ccm unaijua na inakuja 2015 ili Tanzania ibaki na uhai
 
Tatizo kubwa ni kuwatupa pembeni wakulima na wafanyakazi na kuwakumbatia wafanya biashara na wawekezaji. CCM haiwezi kusema tena kuwa inawatetea wakulima, wafugaji na wafanya kazi bali inaenzi wale wanaowanyayasa.
 
Mzee Tupa Tupa,

Fikiria jangili wa pembe za ndovu ndiye mtendaji mkuu wa CCM taifa, msaidizi wake ni kiongozi wa jeshi la uasi; green guard, wabunge kadhaa wa ccm wanatajwa kuhusika na biashara ya mihadarati. Waziri mkuu kupitia serikali ya ccm amehalalisha wananchi kupigwa na polisi na JWTZ. Sasa hicho ni chama cha siasa au genge la wahuni?
 
CCM ni sawa na UKOO WA PANYA. Kwani Baba mwizi, Mama mwizi, Mtoto mwizi, Dada mwizi, Kaka mwizi, Babu mwizi, Bibi mwizi, Shemeji mwizi, Mkwe mwizi. UNABISHA? Sasa tumia dawa itwayo CHADEMA kuangamiza kabisa ukoo huu wa wadudu waharibifu wa mali asili ya nchi yetu. UPATAPO UJUMBE HUU MTARIFU NA MWINGINE
 
Wote ni tatizo awali nilidhani Nape atakioa chama kumbe siye kabisa
 
Chama chetu cha Mapinduzi sasa hakipendwi kama mwanzo wake. Hakiaminiwi kirahisi hata pale kulikokuwa na ngome za chama chetu kama Lindi na Mtwara.Kinalalamikiwa;kinazidi kuchukiwa. Yawezekana kuna tatizo la ki-mfumo...mazoea. Lakini,wapo watu ndani ya chama chetu ambao ndio walezi wa mfumo huo unaosawajisha heshima ya chama chetu. Mkiwa kama watanzania wenye vyama na msio na vyama,ni nani hasa ni tatizo katika CCM yetu? Kwanini? Tusaidieni ili tujirekebishe na kuimarisha chama chetu. Karibuni waungwana! Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
Tatizo ni uchovu ambao umepelekea fikra zote kuganda
 
Mwigulu Nchemba ndiyo tatizo. Hivi hizi sare mpya za ccm zimebuniwa lini na nani kaziidhinisha ndani ya chama? Taratibu kwa matatizo ya huyu Bwana mtazamo wa ccm kutoka nje kinaonekana kama chama kinachoendelea na uhamasishaji na maandalizi ya kukuza vulugu.
attachment.php

Ili jamaa ----- sana
 
Mkuu,matatizo ya ccm ni mengi sana na yapo wazi,mi nafkiri ungeomba tu solution ambapo utashuhudia Majina ya Masheikh na Mapadri yanapendekezwa kama suluhu
 
Tatizo NI KIZAZI CHA PANYA Baba Mwizi, Mtoto Mwizi, Mama Mwizi, Mjukuu Mwizi, Babu Mwizi. Wenye kuibiwa wameshtuka.

Hii imetulia, pia dharau, kiburi, kuua watu ili mbaki madarakani, kutumia dola kuwalinda, kupuuza waliowaweka madarakani, mbaya zaidi kufanya chama ni cha familia,
 
Mimi nadhani matatizo ni hayo,
1.Rushwa na mitandao haramu imetawala kwenye chaguzi zenu,matokeo yake hamchagui viongozi bora bali wale wenye rushwa kubwa na mtandao mpana
2.Vyeo kutolewa kwa kulipana fadhila na urafiki na kwa kuzingatia weredi na uwezo wa mtu,
3.Kulindana na kuoneana haya pasipo na sababu za msingi,
4.Tamaa kali sana ya kumiliki mali kwa njia haramu na za muda mfupi
5.Kuingilia kazi za mihimili mingine na vyombo vyote vya kusimamia haki,sheria na usawa

Kwa ufupi,ugonjwa mnaoumwa HAMUWEZI KUPONA, KUFA ni suala la siku tu,nayo ni October,2015!
 
Tatizo ni nyinyi wenyewe mumeiperekesha nchi imekuwa ya wachuuzi,walalamishi,waongo, waporaji,wakata tamaa ,dharau kwa wananchi,na kupoteza muelekeo poleni
 
Mwigulu Nchemba ndiyo tatizo. Hivi hizi sare mpya za ccm zimebuniwa lini na nani kaziidhinisha ndani ya chama? Taratibu kwa matatizo ya huyu Bwana mtazamo wa ccm kutoka nje kinaonekana kama chama kinachoendelea na uhamasishaji na maandalizi ya kukuza vulugu.
attachment.php

-Ha!ha!ha!ha!ha Super sana. Hiyo combat ni noma sana, you know kama vipi mzee mzima na mbebs wake you know wajipange sana. Naona mkwe naye kando. Wallahi bongo tambararezz

FEMS !
 
Back
Top Bottom