VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Chama chetu cha Mapinduzi sasa hakipendwi kama mwanzo wake. Hakiaminiwi kirahisi hata pale kulikokuwa na ngome za chama chetu kama Lindi na Mtwara.Kinalalamikiwa;kinazidi kuchukiwa. Yawezekana kuna tatizo la ki-mfumo...mazoea. Lakini,wapo watu ndani ya chama chetu ambao ndio walezi wa mfumo huo unaosawajisha heshima ya chama chetu. Mkiwa kama watanzania wenye vyama na msio na vyama,ni nani hasa ni tatizo katika CCM yetu? Kwanini? Tusaidieni ili tujirekebishe na kuimarisha chama chetu. Karibuni waungwana! Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
Mkuu ya kinondoni yamekushinda.CCM nzima ni mbovu,kuna kila dalili kuwa CCM haiwezi kusaidia tena wananchi milioni 45 watanzania,hawana software ya kutatua matatizo,hata wale wanaona wako vizuri kwenye chama ni wale ambao si mafisadi,lkn na wao pia hawana uwezo wa kutatua matatizo ya watu,Kwa hiyo kwa kifupi hakuna anayefaa,hata kama kuna wachache lazima pia wafundishwe software.Magufuli anawezafundishwa software na CHADEMA na akamudu lkn pia mi naona ni mzee