Ata kama uzi sikuwahi usoma, nadhani uliuelewa vibaya. Iko hivi:
Gmail wanakupa uwezo wa kutuma message 50 kwa kila namba ya baadhi ya mitandao hapa Tz (nadhani tigo, na airtel). Kwahiyo ukifungua account yako ya Gmail kwenye PC, unaweza kutuma hizo sms 50 kwa kila namba. Ata kama una namba 100, basi unaweza kila namba kuitumia sms 50, so jumla ikawa SMS 5,000 umetuma. Ikitokea uliemtumia sms tufanye umetuma sms 30 kati ya 50, akajibu ata moja tu, basi ile count inaanza na upya 50. Hivo unaweza chat na mtu hadi asubuhi wewe SMS zako 50 zikabaki vile vile. Ila ukituma zote 50 hajajibu ata moja ndio zinaisha.
Mtu unaemtumia message, inakuja na email yako, hafu inamwambia kama unataka kureply hii message, tumia namba hii: 07********* na akireply inakuja kwenye PC yako.
Huwezi kusoma message za mpenzi/rafiki yako kaka katika Gmail, hayo mambo ya privacy. Pili weka imani tu mambo haya ya kumfuatilia fuatilia mtu daah, hakuna mwanajukwaa atakae kushauri aisee. Taifa bado linakuhitaji.