Msaada namna ya kuongea na Huduma kwa Wateja halotel

K2S7J3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
447
331
Za asubuhi watanzania wenzangu, nimekwangua vocha ya Halotel kwa bahat mbaya namba mojawapo ikafutika hivyo nahitaji kuongea na watoa Huduma kwa Wateja. Nimejaribu kupiga 100 sijafanikiwa kuwapata zaidi ya kupewa maelezo mengine ambayo hayajatimiza haja yangu na sikupata namna nyingne ya kuongea nao. Je kuna uwezekano wa kuongea Nao au Halotel hawana huo utaratibu wa kuongea na Wateja wao?
 
Wiki moja iliyopita nilipata tatizo kama lako kuhusu hao jamaa wa Halotel. Namba yao ya customer care haitoi nafasi ya kuongea na mhudumu moja kwa moja zaidi ya mteja kupokea maelekezo tu kutoka upande mmoja. Hii haijakaa sawa na inaleta usumbufu mkubwa kwa mteja hasa inapotokea kwamba shida ya mteja inahitaji utatuzi kwa kuongea na mhudumu.
 
Hata airtell... Voda ndo naona wana customer care inayoeleweka..
 
Mim imenitokea leo kwa hawa Halotel.. Ukipiga namba ya huduma kwa wateja hamna kipengele cha kuongea na mtoa huduma kwa wateja.. Zaid ya kusikia promo za matangazo yao
 
Back
Top Bottom