Msaada na ushauri wenu

Msaada na ushauri wenu

simchimba

Member
Joined
Jan 20, 2013
Posts
19
Reaction score
0
Wanajf naomba kama kuna yeyote ambaye anaweza kunisaidia au hata ushauri kwa hili tatzo langu;

Nimekuwa tajiri wa huzuni na masikini wa furaha toka nikiwa darasa la pili, nilianza kujitafutia matumizi madogomadogo kama vifaa vyote vya shule hii ni kwa sababu sikuwa karibu na wazazi baba aliondaka na kuniacha kwa kaka kwasababu ya kesi iliyokuwa ikimkabili wilayani Mwanga.

Na kipindi chote ambacho nilikaa kwa kaka sikuweza kununuliwa vifaa vya shule hii ilinipelekea kuanza kujishungulisha na kazi ya uvuvi ktk bwawa la Nyumba ya Mungu, nilitumia siku za weekend na hata siku za shule nikifanya kazi usiku bila kulala then adhuhuri nakwenda shule, nilifanya hivi mpaka namaliza form 4, 2009.Ingawaje kazi hii ili nisababishia kupelekwa mahakamani ana niliachiwa kwa kifungu kidogo nikiwa form3

Sikukata tamaa nikasomea utalii lakini fani hii inatupasa kujua lugha zaid ya1 na mm najua english, pia leseni ya udereva na mm sina fedha za kuongeza lugha wala kusomea udereva.

Naombeni msaada wenu
 
pole sana hop Mungu atakuonesha njia.kwani hasa msaada wako unataka up hapo sijaelewa.
 
aksante mark, kwa sasa nahijitaji kusomea lugha ya kifaransa na kujifunza udereva ili nipate leseni, hii ni kwasababu kampuni nyingi zinahitaji mtu mwenye sifa hzo
 
pengine ushawai sikia sehemu wanakoz nzur ya french.na udereva ni mda gan.upi unataka anza nao.ulishawai omba hata kaz
 
ni Alliance Francaise na favre language & communication institute, vyote viko hapa dar ningependa kuanza na udereva, muda ktk udereva sifahamu , nimeshawai kutuma makumbusho ya taifa kuomba kuwa tour guide na ktk kampuni kule arusha lakini hakuna jibu
 
Aisee rafiki pole sana kwa kweli story yako inahuzunisha sana,pia nakupa hongera kwa kuweza kufika mpaka form 4 licha ya vikwazo ulivyopitia.Nakuona kwa kweli unaplan nzuri za kukuendeleza maisha yako.Kwa upande wagu mie sina msaada wa kuweza kukupa ila ni kukushauri tu usiache kumwomba mungu na siku moja atakufungulia njia.
 
ndugu usikate tamaa ipo cku milango itafunguka,jaribu kubadili maamuzi kama vp jiunge Jeshi la kujenga taifa
 
Aisee rafiki pole sana kwa kweli story yako inahuzunisha sana,pia nakupa hongera kwa kuweza kufika mpaka form 4 licha ya vikwazo ulivyopitia.Nakuona kwa kweli unaplan nzuri za kukuendeleza maisha yako.Kwa upande wagu mie sina msaada wa kuweza kukupa ila ni kukushauri tu usiache kumwomba mungu na siku moja atakufungulia njia.

aksante na siku zote nitamshukuru mungu na kumuomba kwakuwa nilishakata tamaa pale nilipokuwa naudhulia mahakamani na shule kwa muda wa miezi 8 lakini akaniinua nakunipa nguvu tena ya kufanya kazi ile ile na nkafankiwa kulipa ada kwahvyo nitaendelea kumshukuru mungu
 
ndugu usikate tamaa ipo cku milango itafunguka,jaribu kubadili maamuzi kama vp jiunge Jeshi la kujenga taifa

wazo zuri ila ujeshi ilikuwa plani yangu pia lakini wakati nakamatwa na watu waliokuwa wakishirikiana na polisi walinipiga na kasia kwenye mkono na mpaka sasa nahisi hauko salama na muda mwengine huwa unauma sasa kama nitakwenda jeshi sii ninawezashindwa?
 
ada ya udereva ni kiasi gani? Mie pia najisomesha elimu ya juu, nimepitia vikwazo vingi lkn Mungu ni mwema nilifanikiwa kufungua biashara na ndio inanilipia ada na matumizi yangu binafsi. Napenda kukusaidia japo kidogo, ni pm nijue ada ni kiasi gani na inalipwaje kama itakua ndogo nitakulipia yote lkn kama ni kubwa sana nitachangia. Nimeumia sana na nayasikia maumivu uliyonayo. Mimi pia bado ni mwanafunzi lkn nipi tayari kula milo miwili na mmoja nikusaidie wewe japo ada robo au theluthi
 
aksante rafiki duda na nitafurahi sana, ada ya udereva veta rafiki yangu aliniambie yeye alisomea kwa sh.160000 mwaka juzi ila sijui kwa sasa kwani sijawahi uliza nilihofia kuwa hata nikienda kuuliza huku sina pesa ni bure, namna ya kulipa tunaweza kwenda mimi na wewe veta siku ambayo utakuwa na nafasi kwa uaminifu zaidi : namba yangu 0718281024 / 0765259778

masomo mema duda
 
Back
Top Bottom