Msaada na ushauri wa shule/chuo kwa mtoto 'slow learner'

WA MAMNDENII

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2010
Posts
344
Reaction score
58
Wanajamvi nakuja mbele yenu nikiamini hili ni jukwaa lenye msaada na ushauri mkubwa kwa wadau mbalimbali,

Ni hvi, nina chalii wangu umri miaka 15 ambaye yupo std 7 na uwezo wake kwa darasa ni mdogo kupita kiasi ndio maana kwa umri na hilo darasa amekwisharudia mara nyingi sana lakin wapi, sio mtundu na hana tatizo la ulemavu wa akili bali uwezo wake wa kumbukumbu ndo shida, anasoma english medium na ana mwalimu wa tution lakini bado ticha hadi aliamua kuacha kumfundisha kwani aliona no improvement na kunionea huruma kuendelea kulipwa for nothing , mfano mtihani wa muhula uliopita hisabati alipata swali moja kati ya 50 tena la kujumlisha, masomao mengine anajaribu kuotea ya multiple choice lakini ya kujieleza hawezi kabisa hata kuandika sentesi , "INANIUMIZA SANA JOOO"!!! hata shule anayosoma hawajamsajili kufanya mtihani wa std 7 kuwa atafeli hivyo kuirudisha shule nyuma kimatokeo.

Mwezi wa nne mwaka huu nilishauriwa na walimu wake nikampeleka kwa wataalam na walimu wanaofudisha na kutoa ushauri ambao wapo kituo kimoja cha kulea watoto wenye ulemavu wa akili kilichopo mtoni mtongani walimfanyia usaili na walikuta akili ipo ok ila uwezo wa kumbukumbu ndo shida , kiukweli iliniumiza mimi hata yeye mtoto kisaikolojia kwani alifanyiwa usaili na kundi la watoto ambao wote ni walemavu wa akili ( samahani sina nia mbaya kwa hawa watoto ).

Kiukweli huyu chalii hana uwezo wa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza , nimepata ushauri nimpeleke shule/chuo cha ufundi, sijui shule/chuo kipi kwa mdau anayejua inaweza kuwa msaada kwa huyu chalii kwani kumbakisha nyumbani ndo hatari zaidi , tafadhali mwenye ushauri aidha wa shule/chuo hasa boarding itakayoweza kumsukuma kidogo huyu chalii kwnani bado umri ni mdogo sana kuingia mtaani,

sorry kwa maelezo marefu ya kuchosha kwani huyu chalii ananiumiza kinyama na ndie uzao wangu wa kwanza.
 
mchunguze ana kipaji gani Mungu hakunyimi vyote endeleza kipaji chake kiwe ajira yake
 
Muulize akiwa yuko free kabisa nayuko hepi kwamba anataka afanye kazi gani ? Utashangaa atakavyofanya vizuri kwenye hiyo kozi.
Kuna mwanzilishi wa kiwanda cha pikipiki Japan alikua hivyo hivyo, ila babake alipomuuliza nakuambiwa dogo ana interest ya ufundi wa pikipiki, dogo alifanya ufundi mpaka akafungua kiwanda. Hata akikuambia anataka kufuga nguruwe usimcheke. Muendeleze huko huko anakotaka
 
Mimi nina mambo mawili ya kuchangia katika mada hii.

1. Mdogo wangu anayenifuatia alionekana kuwa ana uwezo mdogo darasani. Japo sikwa kiwango hicho unachosema. Nilimrudisha nyuma madarasa na nikawa namtafutia shule nzuri na walimu wa tuition. Akiwa form three mwalimu wake wa tuition akanieleza kwamba niache kabisa kumsomesha nimnunulie gari ndogo afanye biashara ya taxi. Sikuchukua ushauri wake, badala yake niliendelea kumpa encouragement na support. Chuo nilimchagulia BA ambayo nilijua. Hivi sasa yeye ni meneja ofisi flani.

2. Last born wangu akiwa nursery school mpaka standard one, walimu walisema uwezo wake mdogo mno. Kipindi flani nilimuandaa mwenyewe for class tests, alifaulu sana. Nikajua anao uwezo. Akiwa standard 2 tukahamia nchi moja za magharibi. Huku nako walimu hawa wazungu wakasema ana uelewa mdogo. Wakamuandalia wataalam wa child psychology. Costs zote ni kwa serikali. Wakampa mpaka laptop humo waka install programs nyingi za kuinua iq. Hivi sasa anaperform vizuri sana. Lakini principal wa shule alinambia neno moja. Alisema mwanangu hana tatizo ila tumchukulie kama an individual na tumpe support ya kumtia moyo.

3. Nilisoma primary na mtoto mmoja ambaye uelewa wake ulikuwa chini sana. Wazazi wake walijaribu kumrudisha nyuma. Hata sekondari nahisi kuna namna walivyofanya ili itangazwe kafaulu. Ukumbuke huko nyuma tulikuwa na sekondari chache tz. Alipofika form four ikashindikana kabisa. Bado hawakukata tamaa. Walimpeleka kozi za hotel management. Sisi tuliona kwamba huyo kafeli maisha. Hivi sasa yupo state moja USA ni meneja wa hotel.

4 Mwisho, kama wewe ni mkiristo, fanya kila mara hiki nilichofanya na bado nafanya kwa wanangu. Muombee wewe mwenyewe mwanao. Siyo lazima kumwekea mikono, ila huwe una mbariki mwanao kwamba awe na ufahamu mzuri darasani na awe na future nzuri. Sisi wababa tuna power kubwa sana kiroho kwa watoto wetu na kwa mke wetu pia. Kristo ni kichwa cha mume. Mume ni kichwa cha familia. Sikushauri kumpeleka kwenye vituo vya maombi maana hakuna atakaye weza kumuombea kila mara na kwa miezi mingi. Fanya wewe kama umebatizwa. Kila mkiristo aliyebatizwa anao uwezo wa kufungua yaliyofungwa kwa njia ya sala. Mhudumu mmoja USA anaitwa Francis Mcnutt alitunga kitabu kinaitwa Soaking Prayer. Kinakushauri kwamba kama unaona tatizo ni kubwa basi liwekee ratiba ya sala tena fanya hivyo kwa miezi au miaka.Usiweke imani yako kwa wachungaji hao nao wana matatizo yao na wengi wao ni wajasiriamali.

Asante
 
Mtoto wako ni mmoja wa watoto wenye vipaji jaribu kumdadisi anapenda kufanya nn huenda huko ndiko alikopangiwa
 
Mungu akunyimi vyote, mimi nina dogo hapa nyumbani, wenzake alioanza nao std one sa hv wapo form two yeye ndo yupo la saba, yani kichwani zero kabisaaaaa,! Ila sasa ana utundu wa mambo ya electronics, ukiingia chumban kwake kama umeingia TANESCO yan anaweza akatengeneza kitu cha umeme mpk unabaki unashangaa,alishawahi kutengeneza tv mpk ikafanya kazi, sema mfumo wetu wa elimu ya tanzania ni mbovu, wenzetu huko wakiona anakipaji flani, yan huyo wanamchukua fasta wanamwendeleza na kipaji chake,! Kikubwa ukae nae chini then umuulize kitu gan anakipenda.
 
Muulize akiwa yuko free kabisa nayuko hepi kwamba anataka afanye kazi gani ? Utashangaa atakavyofanya vizuri kwenye hiyo kozi.
Kuna mwanzilishi wa kiwanda cha pikipiki Japan alikua hivyo hivyo, ila babake alipomuuliza nakuambiwa dogo ana interest ya ufundi wa pikipiki, dogo alifanya ufundi mpaka akafungua kiwanda. Hata akikuambia anataka kufuga nguruwe usimcheke. Muendeleze huko huko anakotaka
Much thanks mkuu kwa ushauri
 
Mimi nina mambo mawili ya kuchangia katika mada hii.

1. Mdogo wangu anayenifuatia alionekana kuwa ana uwezo mdogo darasani. Japo sikwa kiwango hicho unachosema. Nilimrudisha nyuma madarasa na nikawa namtafutia shule nzuri na walimu wa tuition. Akiwa form three mwalimu wake wa tuition akanieleza kwamba niache kabisa kumsomesha nimnunulie gari ndogo afanye biashara ya taxi. Sikuchukua ushauri wake, badala yake niliendelea kumpa encouragement na support. Chuo nilimchagulia BA ambayo nilijua. Hivi sasa yeye ni meneja ofisi flani.

2. Last born wangu akiwa nursery school mpaka standard one, walimu walisema uwezo wake mdogo mno. Kipindi flani nilimuandaa mwenyewe for class tests, alifaulu sana. Nikajua anao uwezo. Akiwa standard 2 tukahamia nchi moja za magharibi. Huku nako walimu hawa wazungu wakasema ana uelewa mdogo. Wakamuandalia wataalam wa child psychology. Costs zote ni kwa serikali. Wakampa mpaka laptop humo waka install programs nyingi za kuinua iq. Hivi sasa anaperform vizuri sana. Lakini principal wa shule alinambia neno moja. Alisema mwanangu hana tatizo ila tumchukulie kama an individual na tumpe support ya kumtia moyo.

3. Nilisoma primary na mtoto mmoja ambaye uelewa wake ulikuwa chini sana. Wazazi wake walijaribu kumrudisha nyuma. Hata sekondari nahisi kuna namna walivyofanya ili itangazwe kafaulu. Ukumbuke huko nyuma tulikuwa na sekondari chache tz. Alipofika form four ikashindikana kabisa. Bado hawakukata tamaa. Walimpeleka kozi za hotel management. Sisi tuliona kwamba huyo kafeli maisha. Hivi sasa yupo state moja USA ni meneja wa hotel.

4 Mwisho, kama wewe ni mkiristo, fanya kila mara hiki nilichofanya na bado nafanya kwa wanangu. Muombee wewe mwenyewe mwanao. Siyo lazima kumwekea mikono, ila huwe una mbariki mwanao kwamba awe na ufahamu mzuri darasani na awe na future nzuri. Sisi wababa tuna power kubwa sana kiroho kwa watoto wetu na kwa mke wetu pia. Kristo ni kichwa cha mume. Mume ni kichwa cha familia. Sikushauri kumpeleka kwenye vituo vya maombi maana hakuna atakaye weza kumuombea kila mara na kwa miezi mingi. Fanya wewe kama umebatizwa. Kila mkiristo aliyebatizwa anao uwezo wa kufungua yaliyofungwa kwa njia ya sala. Mhudumu mmoja USA anaitwa Francis Mcnutt alitunga kitabu kinaitwa Soaking Prayer. Kinakushauri kwamba kama unaona tatizo ni kubwa basi liwekee ratiba ya sala tena fanya hivyo kwa miezi au miaka.Usiweke imani yako kwa wachungaji hao nao wana matatizo yao na wengi wao ni wajasiriamali.

Asante

Asante mkuu ushauri wako baadhi ya maeneo uliyogusia nilishaanza kuyafanyia Kazi
 
Mungu akunyimi vyote, mimi nina dogo hapa nyumbani, wenzake alioanza nao std one sa hv wapo form two yeye ndo yupo la saba, yani kichwani zero kabisaaaaa,! Ila sasa ana utundu wa mambo ya electronics, ukiingia chumban kwake kama umeingia TANESCO yan anaweza akatengeneza kitu cha umeme mpk unabaki unashangaa,alishawahi kutengeneza tv mpk ikafanya kazi, sema mfumo wetu wa elimu ya tanzania ni mbovu, wenzetu huko wakiona anakipaji flani, yan huyo wanamchukua fasta wanamwendeleza na kipaji chake,! Kikubwa ukae nae chini then umuulize kitu gan anakipenda.

Big up mkuu, thanks
 
Hakuna kitu kama "slow learner"

Huyo mtoto anatatizo la ku lose concentration,kutokuwa focused

Mambo ya kumbukumbu yanakuja with practice.Kuna mental exercise za kuongeza memory ka mnemonics
 
Sijalisoma neno la mwisho chief
 
Moja ya vipimo vya IQ ni uwezo wa kukumbuka(power of recalling) hivyo naweza kusema kuwa kijana wako ana lowest IQ score.

Inaonekana malezi yake ya utotoni hasa lishe haikuwa mzuri na ninyi mkampeleka shule kwa kuangalia umri wake wakati IQ nzuri haitegemei ukubwa wa umri, kwahiyo naweza kujubaliana na hao wataalam waliosema tatizo ni kutokuwa na kumbukumbu.

Nakushauri ukamtengenezea mazingira yanayoweza kuweka sawa kumbukumbu yake na kuvuta muda nako ni vizuri kwani atachukua muda kuelewa yale wanayoelewa wanafunzi wa rika lake.

Watoto kama hao wapo wengi shule zetu hizi za serikali na ndio hao unaosikia wanamaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma na kuandika, na hii inatokea kwa kuwa shule za walalahoi hawapimi uwezo wa mtoto kama kugezo cha kufanya mitihani ndio maana hakuonekani kuwepo tatizo.

Huko veta unakoshauriwa umpeleke nako kunahitaji kumbukumbu nzuri ili aweze kuelewa anachofundishwa. Vumilia tu mtoto atakuwa vizuri baadae. Kama umewahi kusikia kuna watu wamechelewa kukuwa ndio huyo mtoto.
Kama siko sahihi lete taarifa za maendeleo ya mtoto tangu alipozaliwa na kufikisha miaka mitano.
 
Back
Top Bottom