kama kweli ana kilo kumi mbona amepita hata kilo anazotakiwa kuwa nazo kutokana na umri wake kwasababu mtoto wa miezi mitatu anatakiwa kuwa na kilo kuanzia 6 hadi 7 asishuke hapo...kwa hiyo mimi naona anakua vizuri ila nahisi huo atakuwa mtoto wako wa kwanza maana wamama wapya ufikiri unene wa mtoto ndio afya wakati sio kweli...na wengine hufikia kumlazimisha mtoto kula kwa nguvu ili afikie "unene" autakao mama..
Cha msingi hakikisha anakula vizuri na kama anasumbua kula angalia labda position unayompea chakula (kumnyonyesha) haipendi na hivyo kumkera ila hapa sijaona tatizo bali hofu yako tu