Habari za jioni wakuu
Ninaandika hapa nikiwa sina amani kabisa. Mwanangu wa kike miaka 7 anaumwa ugonjwa unaotutisha. Usiku akiwa amelala kuna muda anakoroma sana tena kwa muda mrefu.
Yaani anakuwa ni kama kuna kitu zaidi ya kusinzia kwa kawaida. Akiwa katika hali hiyo hata ukimuamsha vipi haamki. Hata ukimtingisha vipi haamki yaani hata ufanye nini. Baada ya muda kama lisaa au masaa mawili ile hali inaisha anakuwa anatokwa na jasho sana. Ilianza kidogo kidogo ila sasa hali inazidi kuongezeka.
Amekuwa akisumbuliwa zaidi na ule ugonjwa wa kubanwa kifua sijui ndio Limonia. Amekuwa akipewa matibabu anapata nafuu (anapona). Na ana muda yuko vizuri.
Kama kuna mtu anayejua unaweza kuwa ugonjwa gani au tatizo gani naombeni ushauri ndugu zangu, nipo kwenye wakato mgumu.
Natanguliza shukrani