Natumaini humu jukwaan tuna madaktari wazuri na hata watu wengine waliokwisha kutana na tatizo kama langu. mwanangu ana miezi 7 sasa, akicheka sana anapatwa na kwikwi. Mpaka nimeacha kumchekesha kwani namuonea huruma. Nilimuuliza daktari ambaye ni best yangu akaniambia ni kawaida itaisha.
Naomba msaada wenu nimpe dawa gani? Au nifanye nini?