Msaada mtoto wa miaka minne (4) hapendi chakula zaidi ya chai na mikate

masharubu

Senior Member
May 5, 2010
155
10
Wadau naomba msaada mtoto wangu wa miaka 4 na niwa kiume hapendi kula chakula chochote zaidi ya chai na mikate ya boflo.Ukimlazimisha kula kwa nguvu anakula kiasi na baadae anajitapisha.

Nilimpeleka kwa Dkr alitibiwa malaria na kupewa dawa za kupenda kula inaitwa PHAMACTIN lakini wapi hataki kabisa kula, amekuwa kama msomali ukimuona
 
kawaida tu hiyo hata sie tuna kajamaa ka five years yy hata akiwa amelala anaota analilia mkate na chai.. sioni kama ni tatizo.
 
Wadau naomba msaada mtoto wangu wa miaka 4 na niwa kiume hapendi kula chakula chochote zaidi ya chai na mikate ya boflo.Ukimlazimisha kula kwa nguvu anakula kiasi na baadae anajitapisha.

Nilimpeleka kwa Dkr alitibiwa malaria na kupewa dawa za kupenda kula inaitwa PHAMACTIN lakini wapi hataki kabisa kula, amekuwa kama msomali ukimuona

Mkuu umri huu watoto wanasumbua sana kwa chakula...Nililiona hili kwa mtoto wa kaka yangu na ilifikia hatua kama hiyo ya kumpeleka mpaka hospital na daktari alisema inatokea kwa watoto wa umri huo na hakuna haja hata ya kumpa dawa..kubwa cheza na akili yake kwa mfano huyu niliyokupa mfano kwa kuwa muda mwingi nilikuwa niko nae nilikuwa namshawishi kama; 'ukinywa maziwa unarefuka haraka' ukila matunda unakuwa na nguvu kuliko watoto wote' tumia mbinu za aina hiyo kwani ukimlazimisha matokeo yake anatapika then hata kile kidogo anakitoa.
 
Wadau naomba msaada mtoto wangu wa miaka 4 na niwa kiume hapendi kula chakula chochote zaidi ya chai na mikate ya boflo

Katika umri huu kikubwa sio jina la chakula bali ni anachopata kutoka kwenye hicho chakula. Cha muhimu ni kuanza kuupiga soap soap huo mkate, au ku-uPIMP kwa manutrient ya nguvu. Unaweza kujifunza kukanda unga kwa kuchanganya na mayai, dengu, na maprotini mengine.
 
Wadau naomba msaada mtoto wangu wa miaka 4 na niwa kiume hapendi kula chakula chochote zaidi ya chai na mikate ya boflo.Ukimlazimisha kula kwa nguvu anakula kiasi na baadae anajitapisha.

Nilimpeleka kwa Dkr alitibiwa malaria na kupewa dawa za kupenda kula inaitwa PHAMACTIN lakini wapi hataki kabisa kula, amekuwa kama msomali ukimuona

POLE! ENDELEA KUMSHAWISHI MTOTO ATUMIE MATUNDA NA ANGALAU MAZIWA FRESHI PIA WAWEZA PATA CALCIUM YA WATOTO YA TIENS. KM UKIIHITAJI NITAFUTE KWA:-

TEL NO. +255755569494
E-mail: ruhazwentaki@yahoo.com, ruhazwentaki@gmail.com
or visit: http://www.tiens.com, http://www.aftiens.com
 
Jaribu kufuatilia mama yake alikuwa anapenda kula nini pindi alipokuwa na mimba kabla huyo mtoto hajazaliwa! then ndo anza kufanya then ndipo ufuate mautundu aliyokushauri Nduka hapo juu!
 
Ilikuwa ni kawaida yake au ni jambo jipya?
Kama ni jambo jipya mpe dawa ya mnyoo huyo atakuwa na round worm!! na hakikisha unampa dawa kila baada ya miezi mitatu wala huhitaji kupima kwa daktari
 
Mtafutie mafuta ya samaki. Yanauzwa kwenye maduka ya madawa ya binadamu. Yanawaongezea appetite sana watoto.
 
Back
Top Bottom