Msaada! Mtoto mchanga kabonyea upande mmoja

Wild fauna

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
461
189
Salaam.

Nimejaaliwa kupata mtoto mchanga na anatimiza mwezi wa pili kesho kutwa.

Nikiri kwamba huyu ndie mtoto wangu wa kwanza, leo katika kufanya observation ya mtoto nimeona kabonyea upande mmoja wa uso, nimejiuliza sana nikakumbuka huwa tunamlaza kwa tumbo na amekuwa akilalia huo upande wa kushoto uliobonyea.

Naombeni ushauri wenu wana jf, nimekuwa shocked sana sana
 
Salaam
Nimejaaliwa kupata mtoto mchanga na anatimiza mwezi wa pili kesho kutwa. Nikiri kwamba huyu ndie mtoto wangu wa kwanza, leo katika kufanya observation ya mtoto nimeona kabonyea upande mmoja wa uso, nimejiuliza sana nikakumbuka huwa tunamlaza kwa tumbo na amekuwa akilalia huo upande wa kushoto uliobonyea.
Naombeni ushauri wenu wana jf, nimekuwa shocked sana sana
 
Pole sana mkuu.. Mtoto Wa miezi miwili analalia tumbo!? Duh wangu huwa hawakubali!
Ushauri:::: kwanza mlaze mtoto chali hasa usiku( alalie mgongo) mchana umlazie ubavu na sababu ni mdogo mwekee supporting material kwa nyuma asianguke na muwe mnamgeuza ubavu Wa kulia na kushoto, pia mpe vimazoezi vidogo vidogo vya umri wake.

( mkuu nimekuwa nikifanya hivi na sijawahi ona mwanangu amebonyea) hata hivo Mimi sio doctor, wataalamu wakikupa ushauri ni vizuri ukaupokea na kuufanyia kazi.
Kila la heri mkuu.
 
Kuna wamama watu wazima huwa wana namna Yao ya kuwakanda watoto Kama hao..Ila naona kwa sasa Punguza kumlaza huo upande uliobonyea,pia mtoto usimlaze upande mmoja sana,alale upande,alalie mgongo,tumbo pia Ila jaribu kuwa unamgeuza Mara kwa Mara ili abalance...

Pia unaweza mkanda Na mafuta ya Nazi hicho kichwa taratibu,yan Kama unamfanyia massage ya kichwa,inaweza ikasaidia
 
Ingekuwa Ana chogo,ningesema umtengenezee ngata ya kichwa,then akilala kichwa unamdumbukiza Kwenye Ile ngata,sasa sijui huyo wako kabonyeaje...Pole mamie
 
Mh kabonyea vipi, watoto wachanga hutakiwi kuwalaza upande mmoja kila siku sababu viungo viteke.

Kwa case ya uso naogopa kukushauri, ila ingekua kichwa ungechukua mafuta ya nazi na samli ukawa unamkanda kanda inasaidia kuweka kichwa kwenye shape nzuri.
 
Back
Top Bottom