Nimebahatika kufika Bangkok mwezi june, japo sikwenda kwa ajili ya biashara ila nimejionea fursa nyingi.
Kwa upande wa nguo ni very cheap na ni quality, mfano viatu ni kuanzia bht 100 na tshirt na mashati ya maana kuanzia bht 100, jeans na cadet tunazouziwa huku 50 na kuendelea ni kuanzia bht 500, kama utanunua mzigo mkubwa sana utapata punguzo la bei hizo.
Kwa upande wa electronics nimekuta simu nazo ni bei nzur sana japo sijalinganisha na China, mfano note 5 nimenunua kwa bht 15000.
Maeneo ya kufanyia manunuzi nenda Platinum fashion mall(nguo za aina zote, viatu, mabegi), MBK kwa second hand na new electronics, Pantip kwa ajili ya electronics pia, Chatuchak weekend market kwa vitu mchanganyiko, hii sehemu ni sawa na masoko ya mnada yani linaanza ijumaa jioni mpaka jumapili jioni.
Kuhusu malazi na chakula ni bei ndogo sana, chumba ni kuanzia bht 750 kwa maeneo mazur ya Pratunam ambapo hapa hutahitaji usafiri wa kuzungukia maduka yote makubwa niliyotaja hapo juu.
Nimejaribu kueleza kidogo nilichokiona Thailand(Bangkok)