Habari,
Hii ni hali ya kawaida kwa mama aliyejifungua na akaendela kunyonyesha vyema. Wakati wa unyonyeshaji, mwili hutoa kichocheo kinachoitwa Prolactin, ambacho husaidia kwenye kuchochea utengenezaji wa maziwa. Kwa kadri unyonyeshaji unapofanywa vyema kichocheo pia huongezeka.
Kuongezeka kwa kichocheo hiki hutuma ujumbe hasi kwa vichocheo vinavyoandaa mji wa mimba na mayai. Matokeo yake mama huwa hawezi kupata siku zake.
Miili huwa na uwezo tofauti katika hili wengine huweza kupata siku zao lakini wengine huwa hawapati. Lakini pia kuna sababu mbalimbali kikubwa ni kiasi cha unyonyeshaji na mwili wa mhusika.