msaada mke wangu anatapika sana

kayaman

JF-Expert Member
Aug 3, 2013
4,516
10,416
habari zenu wanajukwaa kichwa cha habari kinajieleza, nina mke wangu ambaye ni mjamzito wa miezi mitatu, tatizo amekuwa akitapika sana hasa majira ya asubuhi na jioni na sasa hawezi kunywa maji kabisa na kila akijaribu hata nusu glass anayatapika, anasikia mdomo mchungu sana chakula anakula ila tatizo ndio hakikai tumboni naomba msaada wenu wanajanvi!
 
Hapa tunaweza kukupa ushauri tu mkuu lkn hio inabaki tatizo la kiafya kulingana na condition aliyo nayo! Waone wataalam walioko karibu nawe kwa msaada zaidi, NOTE; Kutapika kunapelekea kupoteza kiwango kikubwa cha maji na electrolytes mwilini na hali hii hupelekea dehydration.... si salama sana usipuuze
 
Hiyo kwa kimedical tunaita hyperemesis gravidarum,,hivyo basi hiyo hali itaisha ifkapo mwez wa nne,,kwa sasa unatakiwa kumpa vitu vya majimaji,kila Mara mpe matunda,,,ukiona hyo hali imezid sana mpeleke hospital,Ila encourage fluid intake kwake,
 
Ajitahidi kula mapema anapoamka tu mana akichelewa kula ngongo inakuwa Kali na inampelekea kutapika sana kutwa nzima , pia aepuke kabisa kula chakula kilicholala au kiporo
 
Back
Top Bottom