Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia kwangu

Mkuu......... ulishawahi kusikia usemi usemao .... Mchumia janga ....".... Pole bana we ulijua kuwa huyo ni mke wa mtu..... ulipaswa kukaa mbali au (to be a wise enough in a foolish way)... to just piga once, twice or thrice and run shaaaaa..... next time be wise joorr (In Nigerian voice).
 
Hivi mtu unaharibiwaje ndoa yako na mtu mwingine bila wewe kupenda, unajua uleolewa kwa nini ukitembeze huko nje. Kama unaona uliye naye si sahihi achana naye. Ni bora mwanamme anaweza kuoa mke wa pili lakini kwa mwanamke huwezi kuolewa na waume wawili.
Mwanamke ni wa kumaumiwa maana anajua kaolewa. Angekataa huyo kijana angekuwa na yeye kimapenzi?
Umeshajua huyu ni mke wa mtu na bwana ake anakutafuta alafu unaendelea naye hiyo ni akili kweli
 
Umeshajua huyu ni mke wa mtu na bwana ake anakutafuta alafu unaendelea naye hiyo ni akili kweli
Huyu bwana ake naye chenga, anatakiwa a deal na mke wake . Huo ni udhaifu mkubwa, hata huyo mke ataendelea kugawa tu maana mwanaume hajielewi.
 
Nasoma huu uzi huku nikiwa na mpango wa kutafuna mke wa mtu. Mipango yote imeshafanyika kuanzia feasibility study. Ila nimeamua kughairi tu, sitaki.
 
Oyass hata mm kuna mazi nakula ila Ana mumewe ni mzeee wa 72 ivii miaka ila mazi mdogo ako na 28 years mnanishauri vip
 
Pole Sana , Ila hiyo ni hatua nzuri ya kujitafakari ili kuwa MTU bora.

Tatizo sio wewe na tatizo sio huyo mwanamke

Tatizo hapo lipo ktk kutojua maana ya useful na important.

Mke wa MTU - ni useful ana manufaa Ila sio muhimu , ni Kama gari na miguu yako , miguu ni important muhimu Ila gari lina manufaa useful.




Ushauri.

Njia ya kwanza nikulikubali tatizo na kuomba msamaha then mwambie ukweli huyo mwanamke kuwa hauwezi kumuoa.

Huyo mwanamke na wewe nyote mmetengeneza hatia (guilty) hivyo kuna Deni tayari mnadaiwa na njia ya kulilipa ni nyie kubadilika na kuwa watu wema.

Kuhusu kufatiliwa na kuuliwa n.k huyo mwanaume hatoendelea kukufatilia maana mke wake. Alikuwa useful na sio important alikuwa Ana manufaa Ila sio muhimu. that's why amekuwa replaced.

"You can't sacrifice someone else's life for ur life there's a karma debt has to be paid"

Tunaweza kuwasiliana , ili upate therapy na kujitoa ktk hatia na kuwa innocence - mnyongofu.
Ushauri mzuri
 
Khabarini wana jukwaa.

Mwaka 2021 nilikutana na dada mmoja mzuri sana, mrembo, mwenye kuvutia na mpole sana ambaye mwanaume yeyote mwenye akili timamu lazima tu angempenda. Basi nikafanya mchakato nikapata mawasiliano yake. Baada ya kuwasiliana na kumueleza shida yangu hakuwa na hiyana hivyo tukaingia katika mahusiano japo alinambia kuwa yeye ni mke wa mtu na ana Watoto wawili.

Kusema kweli tulipendana, mpaka sasa nampenda sana. Mme wake ni mtu wa mishemishe, mara nyingi hayupo. Hivyo nilikuwa naenda usiku kulala kwake na siku nisipoenda basi nilikuwa nampigia simu huyo mpenzi wangu tunazungumza hadi usiku wa manane. Au chatting kwa WhatsApp au sms za kawaida. Japo tulifanya kwa siri sana na mtu asingeweza kugundua, hata rafiki zangu wa karibu hawakujua na rafiki zake pia hawakujua lolote.

Penzi letu lilinoga mno, ilifikia hatua nikawa namiliki CREDIT CARD ya mme wake, na haikuwa issue kufanya miamala midogo midogo. (sio kwamba nilikuwa nalelewa sema tu alinipenda na kuniamini kiufupi tunapendana) pia nilimpenda mno mtoto wake mdogo, nilikuwa nampelekea vizawadi zawadi nikienda kulala, nacheza nako in short ni kacheshi mno kale katoto na kalinipenda pia.

Wakuu, hakuna marefu yasiyo na ncha, hatimaye mwenyemke akajua kwamba mke wake anachepuka, (hapo ndipo chanzo cha tatizo langu) akajaribu kutafuta ajue anachepuka na nani, akatafuta mpaka akapata namba yangu, mke wake akanambia kuhusu hili hivyo tukakubaliana tusitumiane sms na atakuwa ananitafuta yeye. Na mimi niliamua kuchukua extra precaution ikiwa ni Pamoja na kutopokea namba ngeni, pia mke wake alikuwa akinipigia nikipokea nasubiri aanze yeye kuongea ndo na mimi niongee. Baada ya jamaa kuona sipokei namba ngeni wala kujibu sms za namba ngeni aliamua kutafuta jina nililosajiria laini, nashukuru mungu laini yangu hiyo nilisajiri kwa jina la mtu mwingine na mtu huyo alikuwa mkoani hivyo asingeweza kunifahamu.

Baada ya harakati za kunitafuta kugonga mwamba, jamaa aliamua Kwenda mkoani kuendelea na mishe zake. Mimi na mpenzi wangu tukarudisha mapenzi na tukaendelea kuchati na kupeana mambo kama kawaida. Siku ya jumamosi mwezi wa nne tarehe 13 jamaa alirudi, na mke wake alinijuza juu ya ujio wake. Usiku mida ya saa 4 kuna message moja illingia WhatsApp kutoka namba ngeni nanukuu

“NIMEAMUA KUKUACHIA HUYO MWANAMKE, KESHO ATAKUJA MUANZE NAE MAISHA, MIMI NTABAKI NA WANANGU. ASANTE SANA MWANAUME MWENZANGU”

Ujumbe huu ulinishitua sana na ukizingatia ulikuwa umeeandikwa kwa maandishi makubwa kuonesha msisitizo, kusema kweli niliamua kuhama ghetto nikaenda logde kulala ili kulinda usalama wangu maana nilihisi kama naweza patwa na jambo baya. Pia simu nilizima ili isije kuwa tracked nikapatikana kiboya. Usiku sikupata usingizi hata kidogo yaani hata kufumba tu macho hakuna. (acheni jamani watu tunapitia shida sana hapa Tanzania duh) kuna mda natamani hata niwe mkimbizi Afghanistan kuliko kuishi hapa Bongo.

Kuna jambo moja ambalo mke wake hakunambia na alinambia ikiwa ni too late. Kumbe jamaa alimpa zawadi ya simu kabla hajarudi mkoani kwenye mishe zake, simu hiyo alikuwa ameihack achilia mbali normal sms and calls, hata chatting za WhatsApp alikuwa anaziona na kuzisoma. Jambo hili lilinishitua sana maana nilijua atakuwa amenasa pia picture zangu tunazotumiana na mkewe hivyo kudakwa ni suala la muda tu.

Kwa ufupi ni kwamba.

Jana Asubuhi na mapema nilihama huo mtaa, nikaenda mtaa mwingine mbali kabisaa maana nilihisi jamaa anaweza niletea huyo mke wake hadi kwangu. hivyo asubuhi na mapema niliita Kirikuu ikabeba vitu vyangu nikasepa. Leo saa 4 usiku nikapokea simu ya huyu mwanamke (mpenzi wangu) akanambia kwamba

baba jay (code) amekuja na mwanamke mwingine, mimi amenifukuza amekatalia watoto wake nimekuja hapo kwako wamesema umehama, kwanini umehama bila kunambia? Uko wapi nahitaji tuzungumze.

Ujumbe huu umefanya nikatetemeka kuanzia unyayo mpaka utosi, sikutarajia jambo kama hili, huyu mwanamke anasema anataka aje tuishi, pia nimsaidie afungue shauri mahakamani ili apewe talaka, mgawo wa mali na Watoto pia. Yaani niko njia panda nawaza nimuelekeze nilipo? Dah! Hata sielewi… na mimi sina mpango wa kuoa saa hizi. Yaani kimsingi sitaki kabisaa mambo ya kuoa iwe leo au kesho. Hata nikitaka kuoa siwezi oa single mother, nyumbani watanielewaje? Wakiskia story kuhusu huyu mpenzi wangu je itakuwaje? Duh.

Mambo ni mengi sema siwezi Andika yote ntapoteza muda wenu bure.

Ndugu zangu naombeni Mnishauri nina shida sana. Yaani dunia imekuwa chungu sana kwangu, naishi kwa kujificha kama mnyama duh! Nimechoka na maisha ya utumwa. (better die free than living as a slave)

Endelea 👇 👇

Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia Kwangu
Unataka usafiri wa kubeba bitu???bakee
 
Kwa Ushauri tu na Swali juu yako. Ungalikua wewe Ni mke wako anamtaka Mtu unafanyaje. Tafakari Chukua hatua…???!!🤔
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom