Fohadi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2020
- 774
- 2,439
Habari zenu wakuu,
Kiufupi sina historia ya kuwa na matatizo ya masikio na wala sio mtumiaji/ mpenzi wa earphones. Mabadiliko katika masikio yangu nimeanza kuyaona ndani ya kipindi cha miezi miwili iliyopita. Hii hali imekuwa inakuja na kupotea ila kwa hizi weeks 2 imekaa muda mrefu. Iko hivi;
Masikio yanasikia vizuri ila kuna hali fulani strange naiona kwenye masikio yangu. Hali ninayoipata ni kama anayoipata yule mtu aliyekaaa jirani na speakers za mziki mkubwa kwa muda mrefu akitoka hapo lazima kuna sauti fulani kama ya muungurumo au filimbi ambayo atakuwa anaisikia ndani ya masikio yake...sasa kwangu mimi hii ndiyo hali ninayokuana nayo..inaenda mpaka nafikia muda naona kabisa napata maumivu ndani ya masikio..
Nimetumia dawa aina ya BORIC ACID lakini hadi sasa bado sijaona mabadiliko. Ningependa kupata ushauri kutoka kwa wataalamu je tatizo linaweza kuwa nini na ni dawa ipi nzuri inayoweza kunisaidia maana kuna muda natamani hata kuyaziba masikio kwa mikono ili kupunguza ile hali ya kelele na maumivu niipatayo.
Natanguliza shukrani zangu.