Msaada: Masikio yananitesa sana, nimechoka kuchekwa na kudharauriwa

Kaka madenge

JF-Expert Member
Jan 16, 2021
313
572
Nina tatizo la usikivu kidogo yaani sauti inachelewa kufika,

Japo darasani niliko resit mtihani watu huwa wananidharau na kuniona mjinga lakini kiukweli nafaulu kuliko wengi wao.

Inafikia hatua napachukia na nachukia kukaa na watu wengi naona nikae peke yangu hasa hii Open school inapokuwa muda umeisha ndo natulia najisomea kwa amani.

Leo kulikuwa na presentation lakini nilipochaguliwa kwenda ku present kabla hata sijaenda watu wananicheka, nilivunjika moyo sana. Kiukweli nilikuwa nimeandaa presentation nzuri sana na niliumiza kichwa. Lakini matatizo yamekuwa sehemu ya watu kunifanyia mzaha.

Inavunja moyo kwa kweli naona niache tu na mtihani nisifanye.

Nisaidieni kabla sijachukua maamuzi haya.
 
Inferiority complex..... sidhani kama wanakucheka hausikii vizuri, may be utani tu ila kwakua una hiyo shida basi we mwenyewe unajishtukia pole.

Wakicheka nawe ungana nao cheka zaidi yao, maisha ndio haya haya ndugu.
 
Mkuu humkomoi MTU Sana sana unatafuta kuchekwa Zaid

Prove yourself wrong!

Mengine yanapita tu
Marufu kukata tamaa (ingawa naelewa ni ngumu)
 
Unapaswa kuwa positive na kuipokea Hali yako, wao wacheke wasicheke wewe komaa kufanya unachoamini.

Tena ungana nao kufanya nao utani na uchukulie tu ni utani ili maisha yaendelee nao wakose confidence ya kukutania bila kukupa usaidizi.

Talk to them Kama utani waifahamu vema Hali yako ili wapate elimu na kuwasaidia wengine wenye ulemavu. Be positive all the way and never give up sababu ya watu my son.

Wao wanaojiona wazima Wana ulemavu wa kutotambua changamoto yako wakidhani wako salama. Be humble to them my son na Mungu atakutimizia hitaji lako.
 
Kunatofauti kubwa kati ya neno maisha yako na neno maisha yao pia kuna tofauti kati ya ndoto zako na ndoto zao.

Ni ngumu kukubali hali ya kuwa tofauti na wengine lakini jitahidi utumie udhaifu wako kama chachu ya kufanya vizuri zaidi maana mwisho wa siku maisha ni yako na sio yao ma ndoto ni zako na sio zao, wewe ndio wa kuzitimiza.
 
Pole mdogo angu, utazoea tu usijali.

Fanya mtihani wako kwa amani, maisha ni ya mmoja mmoja hao wanaokucheka leo hawatakusaidia chochote mbeleni utakapokwama kwa ajili tu hukufanya mtihani kwakua wanakudhihaki. ukiwa na tatizo linaloonekana dhihaka ni sehemu ya maisha.

Jifunze kujikubali, wewe ni wewe na wao ni wao mdogo angu huku mbeleni utakujaga kujua watu wa aina hio hawanaga impact yoyote kwenye maisha, ni kundi tu la wajinga fulani ambao watakuja kufikwa na mtihani wa maisha kila mmoja kwa wakati wake na mtihani wao utakua mkubwa mno.
 
HAO WANAOKUCHEKA NI KWA AJILI YA HASADA INAWASUMBUA, SONGA MBELE, SIWEZI KUHADITHIA CHANGAMOTO, HESHIMA ITAPATIKANA IKIWA WEWE MWENYEWE NI MWENYE KUJITAMBUA,
WATACHEKA MCHANA WEEE, NA USIKU WATALALA,
WACHA WACHA WASEME
WACHA WACHA WACHEKE
 
Nina tatizo la usikivu kidogo yaani sauti inachelewa kufika ..
Japo darasani niliko resit mtihani watu huwa wananidharau na kuniona mjinga lakini kiukweli nafaulu kuliko wengi wao..

Inafikia hatua napachukia na nachukia kukaa na watu wengi naona nikae peke yangu hasa hii Open school inapokuwa muda umeisha ndo natulia najisomea kwa amani.

Leo kulikuwa na presentation lakini nilipochaguliwa kwenda ku present kabla hata sijaenda watu wananicheka, nilivunjika moyo sana..
Kiukweli nilikuwa nimeandaa presentation nzuri sana na niliumiza kichwa. Lakini matatizo yamekuwa sehemu ya watu kunifanyia mzaha.

Inavunja moyo kwa kweli naona niache tu na mtihani nisifanye..
Nisaidieni kabla sijachukua maamuzi haya.
Pole sana.

Naelewa vizuri unachopitia. Hata mimi ninashida kama yako. Cha msingi, jiamini usiogope watu au kuchekwa utajiumiza zaidi na kuongeza tatizo. Bahati nzuri unafaulu na kufanya vizuri darasani hovyo kuchekwa au kudharauliwa chukulia ni sehemu ya changamoto. Usidhike kuchukia au kukasirika. Fanya tu kile unachoweza na kulicho ndani ya uwezo wako huko shuleni, usichokiweza sababu ya hali yako ya usikivu hafifu omba msaada kwa unaowaamini na kukuthamini au achana nacho.

Zaidi tunagroup la whatsap la watu wenye shida kama yako. Tunashare na kukifunza mengi kuhusu hali zetu za usikivu hafifu

Karibu.
 
Hapo ndio pazuri kuonyesha uwezo wako...

Hao wana maumivu jinsi unavyo wapita wakati wao ni wazima..sasa njia ni kukufanya ujiskie vibaya ili ukwame..

Jiamini ...tena cheka nao vizuri tu.. wataacha huo upuuzi..
 
Hebu jichunguze kwanza!

Huenda muonekano wako ndiyo unawachekesha the way unavyo interact na mazingira yako!

Sidhani kama wanaweza kukucheka kisa husikii vizuri!

Ukijitathmini kwa kina lazima utagundua ipo namna nyingine unayowachekesha..

By the way, hilo tatizo umezaliwa nalo au limekupata ukubwani?

Sent from my SM-J105H using JamiiForums mobile app
 
Chukua bangi mbichi fikinya nyunyuzia maji yake sikioni. Fanya kwa siku3 kutwa mara 3 matonye ma3-4 kila sikio. Ila kama umezaliwa hivyo kaa mbali na ushauri huu
 
Asee una tatizo dogo sana.
Kuna watu wanatukanwa na kusingiziwa vitu vya ajabu ila wanasonga mbele tu.
Hilo tatizo lako ni dogo sana.

Kuna watu hadi wanachukiwa kutokana na maumbile tu ambayo hawawezi kuyabadili.Wewe kama watu wanakucheka,mbona ni jambo dogo sana.Ungesema wanakubagua hiyo ndiyo mbaya sana
Nina tatizo la usikivu kidogo yaani sauti inachelewa kufika ..
Japo darasani niliko resit mtihani watu huwa wananidharau na kuniona mjinga lakini kiukweli nafaulu kuliko wengi wao..

Inafikia hatua napachukia na nachukia kukaa na watu wengi naona nikae peke yangu hasa hii Open school inapokuwa muda umeisha ndo natulia najisomea kwa amani.

Leo kulikuwa na presentation lakini nilipochaguliwa kwenda ku present kabla hata sijaenda watu wananicheka, nilivunjika moyo sana..
Kiukweli nilikuwa nimeandaa presentation nzuri sana na niliumiza kichwa. Lakini matatizo yamekuwa sehemu ya watu kunifanyia mzaha.

Inavunja moyo kwa kweli naona niache tu na mtihani nisifanye..
Nisaidieni kabla sijachukua maamuzi haya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom