Msaada: Masikio yananitesa sana, nimechoka kuchekwa, na kudharauriwa

Kaka madenge

JF-Expert Member
Jan 16, 2021
313
572
Nina tatizo la usikivu kidogo yaani sauti inachelewa kufika ..
Japo darasani niliko resit mtihani watu huwa wananidharau na kuniona mjinga lakini kiukweli nafaulu kuliko wengi wao..

Inafikia hatua napachukia na nachukia kukaa na watu wengi naona nikae peke yangu hasa hii Open school inapokuwa muda umeisha ndo natulia najisomea kwa amani.

Leo kulikuwa na presentation lakini nilipochaguliwa kwenda ku present kabla hata sijaenda watu wananicheka, nilivunjika moyo sana..
Kiukweli nilikuwa nimeandaa presentation nzuri sana na niliumiza kichwa. Lakini matatizo yamekuwa sehemu ya watu kunifanyia mzaha.

Inavunja moyo kwa kweli naona niache tu na mtihani nisifanye..
Nisaidieni kabla sijachukua maamuzi haya.
 
Dahhh
Kuna rafk angu nae anatatizo ka hili but class alikua anafanya vizuri sana
 
Nina tatizo la usikivu kidogo yaani sauti inachelewa kufika ..
Japo darasani niliko resit mtihani watu huwa wananidharau na kuniona mjinga lakini kiukweli nafaulu kuliko wengi wao..

Inafikia hatua napachukia na nachukia kukaa na watu wengi naona nikae peke yangu hasa hii Open school inapokuwa muda umeisha ndo natulia najisomea kwa amani.

Leo kulikuwa na presentation lakini nilipochaguliwa kwenda ku present kabla hata sijaenda watu wananicheka, nilivunjika moyo sana..
Kiukweli nilikuwa nimeandaa presentation nzuri sana na niliumiza kichwa. Lakini matatizo yamekuwa sehemu ya watu kunifanyia mzaha.

Inavunja moyo kwa kweli naona niache tu na mtihani nisifanye..
Nisaidieni kabla sijachukua maamuzi haya.
Pole sana mkuu lakini nakusihi usikate tamaa, unapokumbana na changamoto kama hizo jua kuwa unaenda kushinda hiyo vita ni jambo la muda tu.

Kingine cha kuongeza, nina rafiki yangu nae anatatizo kama lako mkuu na huwa anapata shida sana kwa baadhi ya walimu wenye sauti ndogo hata kama amekaa mbele kusikia ni changamoto.

Aliniambia kuna kifaa maalumu cha kuvaa masikioni kusaidia kusikia kipo kama earphone zile za Masenari nadharia wakuu mshanielewa kwa hapa. Tafuta hiki mkuu utawa prove wrong.
 
Faulu sana fanya presentation nzuri kuliko wao watakuheshimu na kukuogopa wakomeshe kwenye hilo tuuu.
 
Umeenda hospital?

Tafuta hearing aids zitakusaidia temporarily au permanently kama tatizo lako halina tiba.

Pole sana na usivunjike moyo.
 
Pole sana, wapuuze soma kwa bidii ukiamini utafanikiwa na utafika mbali na huo ugonjwa Mungu atakusaidia utapona
 
Achana na hao watu wapuuzi hawajui ya kesho na pia waombee sana dunia sio yetu
 
Pole sana ! Hao wanaocheka achana nao songa mbele kwenye masomo yako, watachekwa wao baadaye wakija kukuona next levels. Ila ulienda hospital? Kuna zile hearing aids wanavaa masikioni zinaweza kusaidia mkuu. Vipi tatizo limeanza ukubwani ama tangu ukiwa mdogo? Polee
 
Pole sana, nenda hospitali wakutibu, na pia mambo ya binadamu waachie wenyewe fanya yako...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom