Msaada: Mabaka ya shingoni na mikononi

makaghari

JF-Expert Member
Jun 20, 2014
534
501
Habari zenu Wana JF,

Nina mdogo wangu (sio wa damu) anasumbuliwa na kinachodaiwa kuwa ni fangasi. Kwa maelezo yake ni kwamba Hali hiyo imekuwa ikimsumbua tangu akiwa mdogo.

Kwanza anapatwa na muwasho hasa maeneo ya shingoni na mikononi. Halafu unamtokea upele. Baada ya siku kadhaa upele hukauka na kuacha alama nyeusi.

Hali hii Mara nyingi humpata hasa akiwa mazingira yenye joto.

Wakati mwingine hata akioga mwili humuwasha Sana Sana tena Sana.

Ndugu zangu naomba mnipe msaada. Je, hao ni fangasi. Na Kama ni fangasi nitumie tiba gani kumsaidia? Na Kama sio fangasi, je, linawezakuwa tatizo gani?

Ametumia dawa za kupaka kwenye ngozi kwa kipindi kirefu, upele unaisha lakini baada ya muda unarudi tena Hali inayomfanya ngozi yake kuonekana kana ina magamba maeneo ya shingoni na mikononi.

Natanguliza shukrani.
 
Habari zenu Wana JF.
Nina mdogo wangu (sio wa damu) anasumbuliwa na kinachodaiwa kuwa ni fangasi. Kwa maelezo yake ni kwamba Hali hiyo imekuwa ikimsumbua tangu akiwa mdogo...
Amphotericin b, fluconazole au griseofulvin.
 
Tafutaaa ketoconazole shampooo na itraconazole capsules zitakusaidiaaaa sanaaaa
Nashukuru Mkuu.

Naomba kuuliza nilikuwa Natumia hiyo Griseofulvin kwasasa takribani siku 13 na sioni Mabadiliko Je, naweza change immediately kwenda kwenye Tiba mpya hiyo Intraconazole Capsules bila kuathiri afya?

Na pia ningeomba unisaidie naweza meza kwa muda gani hiyo Intraconazole Capsules ili kutibu hawa Fangasi Sugu? Ahsante.
 
Nashukuru Mkuu.
Naomba kuuliza nilikuwa Natumia hiyo Griseofulvin kwasasa takribani siku 13 na sioni Mabadiliko Je, naweza change immediately kwenda kwenye Tiba mpya hiyo Intraconazole Capsules bila kuathiri afya?.
Griseofluvin ulikunywa ili utibu fungus gani? Huwaga inachukua muda mrefu sana yani hata week 4 means mwezi mzima kuona results lakini Ukipata na dawa ya Kupata ambayo ni TERBINAFINE bhasi utawahi kuona matokeo mapema.

Ishu ni unatibu fungus gani?
 
Nashukuru Mkuu.
Naomba kuuliza nilikuwa Natumia hiyo Griseofulvin kwasasa takribani siku 13 na sioni Mabadiliko Je, naweza change immediately kwenda kwenye Tiba mpya hiyo Intraconazole Capsules bila kuathiri afya?
Na pia ningeomba unisaidie naweza meza kwa muda gani hiyo Intraconazole Capsules ili kutibu hawa Fangasi Sugu? Ahsante.

Kidonge kimojaaa daily kwa wiki mbili !!! Na shampoo unaogeaaa maraaa 3 kwa wikii fataa maelekezoo utakayopewa then after that utaonaaa matokeoo tuu !!! Change tu
 
Griseofluvin ulikunywa ili utibu fungus gani? Huwaga inachukua muda mrefu sana yani hata week 4 means mwezi mzima kuona results lakini Ukipata na dawa ya Kupata ambayo ni TERBINAFINE bhasi utawahi kuona matokeo mapema.

Ishu ni unatibu fungus gani?
Bahati Mbaya Daktari hakusema Fangasi aina gani.
 
Normally nikiona mtu Ana shida ya ngozi, nachukua picha ya ngozi Yake Kisha naingia kwa Mzee Mwenye Mvi Google, naandika Skin Infection, Skin Deseases... Skin Fungi.. naclick Image Kisha nasearch.

Zitakuja picha nyingi za magonjwa ya ngozi. Nafanya comparison natafuta dawa kwa wazungu nampatia mgonjwa, anatumia anapona.
 
Back
Top Bottom