TCU haitoi majina ya waliochaguliwa. Majina yanatolewa na vyuo vikuu husika. TCU wanachofanya ni kuweka utaratibu mmoja wa kuchagua wanafunzi kwa vigezo vilivyowekwa na vyuo vyenyewe wakizingatia vigezo elekezi vya TCU. Baada ya vigwezo hivyo kukamilika kwa utaratibu wa TCU, basi TCU hupeleka majina kwenye vyuo husika ili wahakiki kama waliochaguliwa wamekidhi vigezo vyao. Vyuo husika wakishajiridhisha ndio wanatangaza majina katika tovuti zao. Inaonekana ndugu yangu hujaelewa maana ya CAS. TCU haina chuo chake kikuu cha kujitangazia majina yake. Ni juu yako kwenda kwenye tovuti za vyuo ulivyopeleka chaguo lako na ukaandikiwa YES, you have met minimum requirement. Kizazi hiki cha Mulugo nacho!!! kazi kwelikweli.