Msaada: Likizo bila malipo.

F35-Bomber

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2017
Posts
1,381
Reaction score
1,119
Habari za mchana wadau wa jf dimbwi la maarifa.
Ninafanya kazi sekta binafsi,nimechukua likizo ya bila malipo sasa ni mwezi mmoja toka October,silipwi mshahara wala chochote kwenye akaunti yangu ya bank ,lakini cha ajabu kuna malipo yanafanyika kwenye mfuko wangu wa kijamii ikionesha kuwa kuna pesa hua inalipwa mwisho wa mwezi kama mshahara kwangu,so utaratibu sahihi ni upi?Binafsi nilitarajia mambo mawili
1: kama pesa yoyote haingii kwenye mshahara wangu basi hakuta kuwa na malipo kwenye mafao yangu ya kila mwezi.
2:kama ni likizo bila malipo basi labfa wanakata pesa yao ya basic lakini stahiki nyingine hunapata kama kawaida.
Sasa nipo hapa nauliza kwa wajuzi wa sheria za kazi ni kipi sahihi,na pia je likizo ya bila malipo ina kikomo cha muda au ikiisha unaweza kuongeza muda au ni vizuri kuresign kabisa.
Nawakilisha samahani nawasilisha.
 
Je, Sera ya Taasisi yako inasemaje juu ya Muda wa Likizo bila malipo? Kwa Upande wa Serikali likizo bila malipo haitakiwi kuzidi miezi 12. Ingawa wadau wamekuwa wakirenew time to time pindi ile miezi 12 inapoisha. Hivyo rejea kwenye sera ya Mwajiri wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…