Msaada: Laptop dell latitude D620 Imezingua

Paul Mchumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2013
Posts
1,043
Reaction score
1,279
Wakuu kama kichwa hapo kinavyojieleza, naomba msaada wa kipi cha kufanya maana laptop yangu tajwa hapo inagoma ku-start inanipa maneno yafuatayo.."No bootable devices--strike F1 to retry boot, F2 for setup utility, press F5 to run onboard diagnostics.", Hii yote imetokana na kuwa leo asubuhi ilidondoka toka juu ya kitanda mpaka chini, baada ya kutaka kuwasha ndio inanipa maneno hayo hapo niliyoyaandika!
 
Hapo kuna mambo matatu;
  • Angalia kama umechomeka usb storage device yoyote, hii inatokea hasa unapokuwa umeset usb storage device kama first boot option kwenye BIOS.
  • PC yako imeshindwa kuisoma Hard-drive yako.
  • Hvyo Hard disk yako imekuwa damaged na hivyo itashindwa kuonekana kama niliposema hapo na. 2
  • Hard disk yako imekuwa imejisplace kutokana sababu kama vile kuangusha

Cha kufanya,
  • Kama ni sababu na. 1, chomoa usb storage ama ingia kwenye BIOS na uangalie kama USB device yako ipo kwenye first priority na uset HDD yako.
  • kama ni sababu na. 2, chomoa chaja na battery kisha ubonyeze power button kwa sekunde zipatazo tano.
  • Kama ni sababu ya mwisho, basi tafuta mtu yoyote mwenye ujuzi afungue na aweze kuangalia tatizo zaidi maana HDD yako inaweza kuwa imesha corrupt.
 
Nimewasoma wakuu,kama HDD imecorrup bei yake inaweza ikawa kiasi gani kwa anaejua,cc DreamChaser
 
Last edited by a moderator:
Nimewasoma wakuu,kama HDD imecorrup bei yake inaweza ikawa kiasi gani kwa anaejua,cc DreamChaser
Sikushauri ufikie hitimisho hapo na kuamua kununua Hard Disk mpya bila kufanya njia nilizokupatia ujaribu. Incase hard disk yako ikawa imecurrupt, bei yake inategemeana kama unanunua mpya au used, na pia inategemeana na makubaliano yenu na muuzaji.
 
Nimewasoma wakuu, kama HDD imecorrupt bei yake inaweza ikawa kiasi gani kwa anaejua,cc DreamChaser

Sikushauri ufikie hitimisho hapo na kuamua kununua Hard Disk mpya bila kufanya njia nilizokupatia ujaribu. Incase hard disk yako ikawa imecurrupt, bei yake inategemeana kama unanunua mpya au used, na pia inategemeana na makubaliano yenu na muuzaji.

Pia inategemea sana na ukubwa wa hard disk anayohitaji, lakini pia huyu amesema tatizo lake limeanza baada ya PC kuanguka na kama hard disk haionekani hivyo uwezekano uliopo yawezekana HDD imetingishika au imekufa.
 
habari wa kuu!na mimi dell yangu imekufa betri natimia direct vp hapo wakuu kunamadhara kufanya hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…