MSAADA: KWA WATUMIAJI WA LUKU

SACO

JF-Expert Member
Jul 25, 2011
2,559
3,298
Habari wakuu...
Ni hivi mimi nipo kwenye kundi la watumiaji wadogo wa umeme. Tatizo kuna baadhi wameniambia kuwa sitakiwi kununua umeme zaidi ya mara moja kwa mwezi, hapa nilipo umeme unaelekea kwisha na mwezi units nilizotumia hazizidi 50 .. Msaada wa haraka unahitajika ndugu kwamba ninunue kidogo hata wa buku 2 au nisubiri (niendelee kuwa gizani hadi tar 1)?
 
Hao wamekudanganya.....hata ununue umeme Mara tano kwa mwezi sawa tu ilimradi matumizi yako kwa mwezi yasizidi 75 units yaani hata uwe na units 100 sawa tu ila usitumie zaidi ya 75 units kwa mwezi

Ikizidi hizo kinatokea nini hebu tiririka mkuu
 
Habari wakuu...
Ni hivi mimi nipo kwenye kundi la watumiaji wadogo wa umeme. Tatizo kuna baadhi wameniambia kuwa sitakiwi kununua umeme zaidi ya mara moja kwa mwezi, hapa nilipo umeme unaelekea kwisha na mwezi units nilizotumia hazizidi 50 .. Msaada wa haraka unahitajika ndugu kwamba ninunue kidogo hata wa buku 2 au nisubiri (niendelee kuwa gizani hadi tar 1)?
Kununua mara moja au mara nne kwa mwezi ni utashi wako kulingana na uwezo wako ki-fedha na energy consumption. Je hao wanaokushauri, kuna kiasi cha fedha wanachangia ili ununue tokens za LUKU?
 
Mimi hawa TANESCO wanadai nipo katika kundi la watumiaji wadogo, lakini cha natumia ghalama kubwa sana kununua units. Wananiuzia sh 350 kwa unit. Je hiyo ni halali kweli?
 
Hv pia kwani ni lazima kununua kila mwezi hata kama unazo za kutosha???
 
Hao wamekudanganya.....hata ununue umeme Mara tano kwa mwezi sawa tu ilimradi matumizi yako kwa mwezi yasizidi 75 units yaani hata uwe na units 100 sawa tu ila usitumie zaidi ya 75 units kwa mwezi
Mwakabanje: issue siyo utumie units ngapi, kwa watumiaji wadogo wasinunue Umeme zaidi ya Tsh 9,000/= Mimi nilinunua Umeme wa Tsh 10,000/= ambao niliutumia kwa siku 43. Niliponunua tena wa Tsh 10,000/= nikapata units 28.7 badala ya units 63 na points. So issue siyo matumizi bali usinunue zaidi ya Tsh 9,000/= kwa mwezi. Sijui kama nimeeleweka.
 
Naomba hapo kwa wemma niongeze na kurekebisha

Kwa maelezo yako upo tarrif 4
Nikimaanisha hapa unauziwa unit 1 kwa shiling 100 kwa hivyo ukitaka kununua umeme nenda na sh 9700 ili uweze kupata unit 75 uzitumie ndani ya mwezi mmoja. Kama ukimaliza unit zote 75 ndani ya mwezi basi kila unit moja utauziwa sh 350.

Kama utazidi unit 75 kwa miezi mitatu TANESCO watakuamisha kutoka tariff 4 wakupeleke tariff 1 ambayo unit moja utauziwa shilling 292.

USHAURI WANGU
Kila mwezi nunua umeme wa sh 9700 ambapo utapata unit 75. Tumia umeme wako vizuri na uhakikishe hauishi kabla ya mwezi kuisha.
Kama ukiisha kabla ya mwezi na ukinunua tena basi badala ya unit moja wakuuzie sh 100 sasa watakuuzia sh 350. Na kama ukiendelea hivi kwa miezi mitatu basi watakupeleka tariff 1 ambayo utauziwa unit 1 Shiling 292

ASANTE
 
Mwakabanje: issue siyo utumie units ngapi, kwa watumiaji wadogo wasinunue Umeme zaidi ya Tsh 9,000/= Mimi nilinunua Umeme wa Tsh 10,000/= ambao niliutumia kwa siku 43. Niliponunua tena wa Tsh 10,000/= nikapata units 28.7 badala ya units 63 na points. So issue siyo matumizi bali usinunue zaidi ya Tsh 9,000/= kwa mwezi. Sijui kama nimeeleweka.
Kweli Tanzanian bado tuko nyuma sana
Pesa n yako lakin unapangiwa
Na matumiz ya kutumia
 
Back
Top Bottom