Msaada kwa wanaojua sheria, Akipatikana na kosa adhabu yake itakuwa ipi?

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
8,923
16,827
Kuna ndugu yangu wa kike kampiga mpangaji mwenzie wa kiume na kumjeruhi na mawe.

Sababu za ugomvi wao ni kurushiana maneno ya maudhi na ndipo huyo mdogo wangu alipokasirika na kumrushia mawe.

Jamaa aliyerushiwa mawe ameenda police na kesi iko mahakamani saiv baada ya mdogo wangu kuonyesha dharau za kutotaka maridhiano na jamaa.jamaa alitaka arudishiwe gharama zake za matibabu tu kama elfu 50 ila dogo kajifanya mjuaji.sasa hivi yuko nje kwa dhamana ya laki mbili na week ijayo ndio kesi inatajwa tena.

Je kuna namna tunaweza kumnusuru huyu dogo na je mfano akipatikana na hatia adhabu yake itakuaje maana shtaka lake aliloshtakiwa nalo ni kushambulia na kudhuru mwili?
tusaidiane wakuu.
 
Kosa: Shambulio la mwili
Adhabu: 241. Mtu yeyote ambaye anafanya shambulio linalosabisha dhara mwilini atakuwa anatenda kosa na atawajibika kwa kifungo cha miaka mitano

Sio mim sheria hyo so mjiandae
 
Kosa: Shambulio la mwili
Adhabu: 241. Mtu yeyote ambaye anafanya shambulio linalosabisha dhara mwilini atakuwa anatenda kosa na atawajibika kwa kifungo cha miaka mitano

Sio mim sheria hyo so mjiandae
duh.mkuu tunafanyaje kumnusuru?
 
Kuna viumbe wanapenda kesi mpaka wanaboa, Huyo ulimchelewesha sana ungemtwisha ya kutaka kumbaka Huyo mdogo wako mwenyeweeee angesema pooo.
 
kuna ndugu yangu wa kike kampiga mpangaji mwenzie wa kiume na kumjeruhi na mawe.sababu za ugomvi wao ni kurushiana maneno ya maudhi na ndipo huyo mdogo wangu alipokasirika na kumrushia mawe.jamaa aliyerushiwa mawe ameenda police na kesi iko mahakamani saiv baada ya mdogo wangu kuonyesha dharau za kutotaka maridhiano na jamaa.jamaa alitaka arudishiwe gharama zake za matibabu tu kama elfu 50 ila dogo kajifanya mjuaji.sasa hivi yuko nje kwa dhamana ya laki mbili na week ijayo ndio kesi inatajwa tena.
je kuna namna tunaweza kumnusuru huyu dogo na je mfano akipatikana na hatia adhabu yake itakuaje maana shtaka lake aliloshtakiwa nalo ni kushambulia na kudhuru mwili?
tusaidiane wakuu.
Shambulio la kudhuru mwili.... search utaona adhabu yake. Pia unaweza serach defence yake!


SURA YA ISHIRINI NA TANO

MASHAMBULIO


Shambulio la

Kawaida 240. Mtu yeyote ambaye bila ya halali anamshambulia mtu mwingine

atakuwa anatenda kosa na , iwapo shambulio hilo halikufanyika katika

mazingira ambapo adhabu kubwa zaidi imetolewa katika Kanuni hii,

atawajibika kwa kifungo cha mwaka mmoja.






Shambulio

linalosababisha

madhara ya

mwili 241. Mtu yeyote ambaye anafanya shambulio linalosabisha dhara

mwilini atakuwa anatenda kosa na atawajibika kwa kifungo cha

miaka mitano.
 
Mleta mada,hiyo kesi inazungumzika,fanyeni kabla ya tarehe ya kesi mumfuate mlalamikaji mmuweke sawa.mwambie huyo dogo aache kisirani cha kijinga,akicheza anaenda magereza kimzaha mzaha tu.
 
Huyo ni wa kufunga tu, na hiyo ndiyo sababu Magereza yapo kwaajili ya kuwahifadhi watu vimeo kama huyo mdogo wako.

Watu wengi hufanya mzaha na Mahakama, mpaka siku Hakimu akimtwisha mvua ndipo akili itamkaa sawa. Mahakama au Sheria haina jambo dogo na wala haina mchezo!

Na mkumbuke hiyo ni kesi ya jinai hivyo ni kesi ya Jamhuri, mlalamikaji yeye kazi yake ni ndogo tu kwenda kuisaidia tu Jamhuri kuipa ushahidi basi.

Asiyefunzwa na *****................. acha akaliwe na Manyapala.
 
Back
Top Bottom