MSAADA KWA WALIMU WOTE

hashimrashidy

Senior Member
Sep 11, 2015
197
145
Habar zenu wakuu,

matumain yangu ni wazma na afya tele naombeni mniuze hili nina kijana ambaye kamalize form 4 na anahitaji kujiunga na ualimu yani kuwa mwalimu kwa ngazi ya chet Naombeni mnijuze je ni vigezo vipi vinahitajika kujiunga na mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya cheti......????

Pia naombeni ufafanuzi juu ya hili Nilitembelea website ya wizara nkaona tangazo lao hili "
KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA KIPINDI CHA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017



Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yaani “Online Central Admission System (CAS)”, umefunguliwa rasmi tarehe 23 Januari, 2017, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi ya mwombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada na Stashahada kwa Kipindi cha Machi/April, 2017 kwa mwaka wa masomo 2016/2017.



Namna ya Kufanya Maombi

Maombi yote yafanyike kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) au kupitia chuoni ambapo mwombaji anapendelea kwenda kusoma, ambapo chuo kitamdahili mwanafunzi husika kwenye mfumo wa udahili kupitia “Institutional Panel”.



Tanbihi: Waombaji wa kozi za Afya waliohitimu Astashahada (NTA Level 5), pia wataomba kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu.

Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo:

  1. Biashara, Utalii na Mipango, mfano; Uhasibu, Meneja Rasilimali Watu, Wanyama Pori, Mipango.
  2. Sayansi na Teknolojia Shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya Mawasiliano, Usanifu Majengo, Mifugo.
  3. Afya na Sayansi Shirikishi, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi.
Sifa za muombaji

  1. Awe amehitimu kidato cha nne mwaka 2015 au kabla ya hapo.
  2. Awe na Astashahada ya mwaka 2016 au kabla ya hapo kwa wanaojiendeleza.
  3. Sifa kwa kozi mahsusi ziko kwenye mwongozo wa kozi (Guidebook) ulioko kwenye mfumo (CAS).
Ada ya maombi ni kama ifuatavyo:

  1. Kwa eneo la Afya na Sayansi Shirikishi ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
  2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=.
  3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Biashara, ada ni Tshs 30,000/=, ambapo muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.
Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 06/03/2017.

Muhimu: Hakutakuwa na muda wa nyongeza wa kufanya maombi. Hivyo waombaji wanashauriwa kuwa makini wakati wa kufanya maombi yao.

Angalizo: Kwa eneo la Mafunzo ya Ualimu na kozi ya Muhudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (Community Health Workers) hayatakuwepo kwenye udahili wa awamu hii."

je kwa wanafunzi waliomaliza mwaka 2016 je wanaweza kuomba wakati huu au kuna awamu inginee.........????
 
Actually umeshafanya searching ya kuhusu maombi ya ualimu na majibu yapo mwishoni. Kitu cha kufanya kwa sasa ni kuvuta subira hata watakapo tangaza kutuma maombi kwa kozi uitakayo.
Kwa kozi ya ualimu ngazi ya cheti unatakiwa kuwa na div 1 hadi 3. Hata ukiwa na sifa pia inategemea na ushindani na nafasi zilizopo kwenye vyuo husika.
 
mm nngekushauri tembelea chuo chochote cha ualimu kilichokarbu nawe kwa msaada zaid,
 
Ili ajiunge na mafunzo ya Ualimu anatakiwa kuwa na division 1 hadi 3.
 
Back
Top Bottom