Msaada kwa waenda kwa miguu!

Msaada kwa waenda kwa miguu!

Joined
Sep 7, 2014
Posts
89
Reaction score
31
Salama wana jf,
Ningependa kutoa mawazo yangu hasa kuhusu watumiaji wa barabara hasa kwenye maeneo ya pundamilia ama zebra, kumekuwepo na namna tofauti ama uelewa tofauti kwa baadhi ya matumizi sahihi ya eneo hilo, kuna watu wanalitumia kwa kupita bila kuwa na tahadhari yoyote, mtu anakata barabara kwa mwendo wa taratibu mno au pia kuanza kuonesha namna ya ufundi wa kutembea, na ukizingatia tupo katika wimbi hili kubwa la waendesha pikipiki wasiotambua ama kuzielewa alama za barabarani na inawezekana pia hawapendi kujifunza sheria za uendeshaji salama!
Nimeshuhudia mara kadhaa ajali ambazo zingeweza kuepukika kwa watumiaji wa barabara, je ni elimu ipi ama njia zipi zitumike ili kuweza kuwasaidia watumiaji wa barabara? Naomba mchango wenu ili tuweze kunusuru maisha ya watanzania wenzetu kwani hapa jukwaa lenye watu wenye uelewa mbalimbali.
Asanteni.
 
Kwanza la muhimu naona kuna umuhimu wa watu kulalamika! Kwanza maana ya muenda kwa mguu ni mtu yeyote katika eneo husika lazima anakuwa mwenda kwa miguu!! Bila kujali anamiliki prado au usafiri wa aina yoyote binafsi! Hivyo ni wakati tu unatofautiana!! Huwezi kuingia na gari lako dukani kutafuta mahitaji!!! Hivyo basi ni muhimu kwa wasanifu wetu kuweka umuhimu wa kila barabara@ inayojengwa iwe na sehemu ya watembea kwa miguu!! Ila naona hili linasahaulika sana! Ni muhimu kuwakumbusha hata kwa lazima!
 
Back
Top Bottom