Msaada: Kwa njozi hii

sir j

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
315
210
Heshima kwenu wana jamvi.
Usiku wa kuamkia leo 'nimeota' njozi ambayo imekifarakanisha kichwa changu mpaka muda huu........

Nimemuona mheshimiwa Lowasa akiwa kwenye halaiki ya watu, ni kama alikuwa kwenye harakati za kampeni (sina uhakika, ingawa kulikuwa na watu wengi mno). Lakini katika hali ya kushangaza, he was poisoned by an unknown person......kuja kustuka, kalegea anataka kuanguka.....watu si ndio kumdaka. Jitihada za kumuwahisha hospitali zikafanyika. Kumfikisha hospital, na vipimo vilipofanyika, vikaonesha tayari keshatutoka......tena kwa sumu kali, iliyomshambulia sana ndani ya muda mfupi tuu......

Nimeamka ndugu zangu hata sijielewi yani....kwamba kwa nini niote ndoto ya namna hii, wakati hata sikulala nawaza wala kufikiri mambo ya wanasiasa...??
Embu mnisaidie kwa wale wajuzi wa kutafasiri na kupambanua ndoto/njozi.

Asanteni sana.....
 
Inawezekana tiss wamekuotesha nini wanatarajia kufanya kwa watu wanaokubalika na wananchi
 
Kapime mkojo kabla hujapimwa kwa kushinikizwa

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Heshima kwenu wana jamvi.
Usiku wa kuamkia leo 'nimeota' njozi ambayo imekifarakanisha kichwa changu mpaka muda huu........

Nimemuona mheshimiwa Lowasa akiwa kwenye halaiki ya watu, ni kama alikuwa kwenye harakati za kampeni (sina uhakika, ingawa kulikuwa na watu wengi mno). Lakini katika hali ya kushangaza, he was poisoned by an unknown person......kuja kustuka, kalegea anataka kuanguka.....watu si ndio kumdaka. Jitihada za kumuwahisha hospitali zikafanyika. Kumfikisha hospital, na vipimo vilipofanyika, vikaonesha tayari keshatutoka......tena kwa sumu kali, iliyomshambulia sana ndani ya muda mfupi tuu......

Nimeamka ndugu zangu hata sijielewi yani....kwamba kwa nini niote ndoto ya namna hii, wakati hata sikulala nawaza wala kufikiri mambo ya wanasiasa...??
Embu mnisaidie kwa wale wajuzi wa kutafasiri na kupambanua ndoto/njozi.

Asanteni sana.....
Usiku kabla ya kulala ulikula nini na ulikunywa nini na kiasi gani na je ulivuta nini?, chumba ulicholala kilikuwa na hewa ya kutosha na je ulioga kabla ya kulala? JE ulilala na nani na mlifanya nini kabla ya kulala? Je ulilala kwako au gesti?
 
mara nying ndoto ukiota huwa kinyume chake!ndoto inakuja kimafumbo fumbo hyo!hv kati ya EL na( PJ wa clouds fm) nan anafanya sana MIKUTANO! mie toka uchaguz uishe sijamuona EL akifanya mikutano!
 
Kwa wale ambao wanaombea sana Taifa, miezi ya karibuni kumekuwa na mzigo mzito sana wa kuombea Taifa. Udhalimu unaotendeka kupitia viongozi na raia wakahuzunika hakika Mungu anasikia kilio na masikitiko ya wenye haki.

Mauji ya kibiti kwa damu isiyokuwa na hatia, hakika hiyo damu inalia kwa Mungu ili ipate haki. Damu hudai ila kwa pampoja twaweza kuomba Toba juu ya hii damu maana ipo damu inayofuta kila aina ya udhalimu, ipo damu inayorehemu. Hakuna damu nyingine zaide ya Yesu.

Kuhusu Ndoto yako sio jambo la kupuuzia maana tunaona ni kweli kabisa haki haitendeki, chuki, ukabila, mabavu n.k vinaonekana waziwazi

Sasa hayo yote yanayotendeka sasa mwisho wake uvunjifu wa amani.

KISASI/HUKUMU NI JUU YA MUNGU.
 
Heshima kwenu wana jamvi.
Usiku wa kuamkia leo 'nimeota' njozi ambayo imekifarakanisha kichwa changu mpaka muda huu........

Nimemuona mheshimiwa Lowasa akiwa kwenye halaiki ya watu, ni kama alikuwa kwenye harakati za kampeni (sina uhakika, ingawa kulikuwa na watu wengi mno). Lakini katika hali ya kushangaza, he was poisoned by an unknown person......kuja kustuka, kalegea anataka kuanguka.....watu si ndio kumdaka. Jitihada za kumuwahisha hospitali zikafanyika. Kumfikisha hospital, na vipimo vilipofanyika, vikaonesha tayari keshatutoka......tena kwa sumu kali, iliyomshambulia sana ndani ya muda mfupi tuu......

Nimeamka ndugu zangu hata sijielewi yani....kwamba kwa nini niote ndoto ya namna hii, wakati hata sikulala nawaza wala kufikiri mambo ya wanasiasa...??
Embu mnisaidie kwa wale wajuzi wa kutafasiri na kupambanua ndoto/njozi.

Asanteni sana.....
Dah aisee naona Mungu kakubeba maana umeota kupitia mlengo wa kushoto,la kama ungeota kupitia mlengo wa kulia du ungekuwa unatafutwa kila kona saa hizi "ndoto ya rema" ila kuwa na amani pako poa tu,
 
Usiku kabla ya kulala ulikula nini na ulikunywa nini na kiasi gani na je ulivuta nini?, chumba ulicholala kilikuwa na hewa ya kutosha na je ulioga kabla ya kulala? JE ulilala na nani na mlifanya nini kabla ya kulala? Je ulilala kwako au gesti?

Kwani njozi/ndoto hutegemea vyote hivi...??!!
 
Tafsiri ya ndoto yako ni hii;

Lowassa amewakilisha maoni na mitazamo iliyo tofauti na utawala uliopo madarakani.
Hiyo poison ni sera na mikakati ya maksudi iliyopangwa na inayoendelea kupangwa dhidi ya mitazamo na maoni tofauti dhidi ya ile ya watawala hawa.

Kinachooneka kutakuwa na siasa za tofauti sana na tulizozoea huko tuendako ambapo demokrasia na haki vitapewa tafsiri mpya. Nahili litamgusa kila mtu katika siasa, aliye mpinzani, mwana CCM na hata mwana harakati.
 
asante mkuu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom