Msaada kutrack iPhone iliyoibiwa

kkenzki

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2012
Posts
1,503
Reaction score
2,514
Wadau habari za sikukuu, niende moja kwa moja kwenye mada. Naandika kwa niaba ya ndugu aliibiwa iPhone β˜“ juzi na boda boda akiwa kwenye foleni maeneo ya Tabata hivyo tunaomba msaada kama kuna mtu anaweza tusaidia namna ya kutrack mpaka kuipata hata kwa malipo tafadhali.
 
Uwezekano wa kupatikana kwa sim hako upo swali je imei ya sim unaijua
 
Huitaji kumfuata mtu inbox wala nini fanya hivi...
Kama alikuwa ka enable find my iphone
Tafta simu ya iphone au ipad fungua app ya find my iphone
Kwenye username aweke email aliyoiset kama icloud ya hiyo iphone x
Passowrd pia ajaze password ya hiyo icloud
Ita search na kuwaonyesha simu ilipo endapo itakuwa imewashwa na ina line.
Kuna option ya kuilock kama atakuwa hakuiwekea lock unaweza ilocate na kuweka any messee kwenye lock screen pia kuna option ya kufuta kila kilichomo kwenye hiyo simu, hii usiitumie kwa maana ukifuta hutaweza kuifuatilia tena.
Kuna pia option ya kufanya iite mfano kama unaitafta umei mispalace ndani.
Kama hauna iphone au ipad au comp ya mac basi waweza fungua icloud.com uka sign in pia utaweza illocate.
Kumbuka usipoiona ujue sim imezimwa au hajaweka line so haisomi inernet.
So simple
 
Vipi kama akienda TCRA hawezi kuipata kiurahisi zaidi?
 
Kwa mara nyingi watumiaji wa iphone huwa ni wale wale walioanzia kwenye 4 au hata 5, ikiwezekana hata 6. Sasa inakuaje mtu anatumia iphone x halaf hajui hata kuaccess "find my iphone" anyway fuata maelekezo ya mtafuta maish hapo juu utafanikiwa.
 
Mbona unabatisha mzee mtu ataweza vip kuweka line kwenye sim ambayo ameiiba
Kwa vyovyote vile hiyo lazma iwe haina internet
 
Mbona unabatisha mzee mtu ataweza vip kuweka line kwenye sim ambayo ameiiba
Kwa vyovyote vile hiyo lazma iwe haina internet
Kwahiyo simu ikiibiwa uwa haiwekewi line?
Nakwambia kitu ambacho nimeswahi kufanya mtu anaweza iba simu asiitoe line wala kuizima niliibiwa ipad ni kaitrack kwasababu aliyeiba hakuizima wala kuitoa line nikamkamata boko basiaya akiwa saluni.
Kuna jamaa yule ilikuwa story kubwa miaka kadhaa nyuma gari ilipasuliwa kioo akaibiwa iphone na laptop yake akaitrack simu yake akaona iko kwenye move from mwenge njia ya bagamoyo road kuelekea tegeta akawaita manjagu wakaifuatilia mpaka wakawakamata wezi na mmoja alikuwa mtoto wa kuadapt wa aliyekuwa raisi wa zenj Salmon Amour.
So huenda aliyeiba anaweza kuwa hajatoa line na huenda aliyeiba anaweza kuwa kaweka line yake akijaribu kuiunlock simu aitumie.
Tena kwa simu kama iphone watu wengi hawana ujuzi nazo
 
Hutaipata maana inaenda chinjwa
Wanatoa battery, housing na kiooo, vingine vinatupwa maana kuna waliovunja vioo vya X zao.
 
Ukiibiwa IPhone we kanunue mpya maana wezi siku hizi wajanja. Wanaenda uza hata 100000 maana haiwezi tumika tena
 
Mkuu nenda katangaze dau kwa bodaboda tu wakurudishie na kuwaeleza tu hawezi kuitumia mtu atakamatwa hivyo kimjinimjini tangaza dau vinginevyo utaitwa inbox utatapeliwa bure, jaribu kama alivyoshauri mtafuta-maisha alivyokushauri kwenye post yake #6.
 
nakushauri karipoti police, utaipata mara moja kuna kitengo cha intelijensia watakusaidia, hulipi hata senti tano na simu unaipata ndani ya masaa 6, watu wa huku mtandaoni wanakudanganya museee. kila la kheri bossπŸ˜±πŸ˜±πŸ˜›πŸ˜›
 
Kwa mara nyingi watumiaji wa iphone huwa ni wale wale walioanzia kwenye 4 au hata 5, ikiwezekana hata 6. Sasa inakuaje mtu anatumia iphone x halaf hajui hata kuaccess "find my iphone" anyway fuata maelekezo ya mtafuta maish hapo juu utafanikiwa.
unaweza kuta hata I cloud hakua na account na find my iphone iko off hapo ahesabu maumivu tu
 
unaweza kuta hata I cloud hakua na account na find my iphone iko off hapo ahesabu maumivu tu
Jinsi nilivyoona tu atakuwa amenunua hiyo simu kama fashion, kiukweli iPhone inatakiwa angalau uweze kuwa mwenyeji wa simu smartphone na mambo ya electronic ndo ina raha kwa upande wa security vinginevyo uitumie kawaida tu ikiibiwa basi unakubali matokeo. Maana mwizi akiiba anatakiwa apate lesson kwamba hizi simu sio za mchezo mchezo lakini kama akiiba alafu ikatumika tena hapo ni kasheshe
 
Natafuta fundi mzuri wa iPhone upande wa charging system
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…