Retards Finder
JF-Expert Member
- Apr 24, 2018
- 509
- 706
Heshima kwenu wanajukwaa.
Muda mrefu sana nimekua na ndoto za kuwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) punde nitakapomaliza elimu yangu ya juu.
Hivyo siku zote nimekua nikiamini siku moja nitakuja kutimiza ndoto yangu ya kuwa askari wa JWTZ. Sikuwa nawaza kuwa mwanajeshi ili tu kuepukana na changamoto ya ajira bali ni kitu ambacho napenda kutoka moyoni,sikuwahi kufikiria kufanya kitu kingine baada ya kumaliza masomo zaidi ya kuwa mwanajeshi.
Ila hivi karibuni nimekuja kukatishwa tamaa ya kufanikiwa kuishi katika ndoto yangu hii mara baada ya JWTZ kubadiri umri wa unaohitajika kwa mtu kuweza kuwa na sifa ya kuwa askari wa JWTZ,kwasasa umri unaotakiwa ni miaka 18 mpaka 25,mabadiriko haya yamenikatisha tamaa sana. Pia mabadiriko haya yatawanyima nafasi wahitimu wengi sana wa Vyuo Vikuu kujiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
Kwasasa nina umri wa miaka 25,natimiza umri wa miaka 26 Februari 2019.
Serikali ya JMTZ na uongozi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), jaribuni kupitia upya mabadiriko haya mliyoyafanya. Yanatunyima nafasi wahitimu wa Vyuo Vikuu Tanzania kujiunga na Jeshi letu PENDWA ili kulitumikia Taifa.