Password
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 777
- 1,082
Habari wakuu.
Mimi ni mmoja wa wanaosubiria kufanya maombi ya kujiunga na elimu ya juu(vyuo vikuu),nimekuwa nikitembelea tovuti(website) yao Mara kwa Mara kuona kama kuna updates zozote juu ya nafasi za masomo kwa waombaji wa mwaka 2017/2018.
Hatimae,jana wametoa update moja inayosema kwamba "maombi yote ya nafasi za masomo yatafanyika moja kwa moja kupitia vyuo husika,isipokuwa kwa wale wanaohitaji kujiunga na kada za afya na ualimu,hao wanaweza kutuma maombi kupitia website ya NACTE yenyewe.Mimi ninahitaji kujiunga na kada ya uhandisi nikianzia ngazi ya diploma,hivyo nikaamua kutembelea website ya DIT,
Lakini kwenye website hiyo kitengo cha kutuma maombi na wao wanasema maombi yote yafanyike kupitia website ya NACTE via CAS(Central Admission System) lakini pia DIT hawajatoa update za mwaka wa masomo 2017/2018 wao bado wanayo maelezo ya mwaka wa masomo 2016/2017,
Nikaamua kutembelea website ya MUST(Mbeya University of Science and Technology) huko pia mambo yapo kama DIT bado hawana update za mwaka wa masomo 2017/2018 na wao bado wapo 2016/2017 ila hawa hawajaeleza pia update zifanyike wapi.
Najua humu ndani kuna kuna wazoefu wengi na pengine wahusika wa system mpo humu,ninaomba ufafanuzi zaidi na pia ushauri nifanye nini baada ya hapo.Ninatanguliza shukrani za dhati kwa wote mtakaotoa muda wenu kujibu na kunishauri juu ya hili,Asanteni.