Heshima kwenu wakuu,
Kwanza ningependa kukiri kwamba Mimi ni Mgeni sana humu jamiiforum lakini nawaheshimu sana wadau na naamini nitapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwenu.
Mimi ni mfanyabiashara Mdogo na nina frame ya biashara katika moja ya miji ya tz. Wakati naanza biashara nilifata taratibu zote ikiwa ni pamoja na zile za tra. Wakati Huo mtaji wangu ulikua mdogo sana (tsh 1m) hivyo pia nilikadiriwa kiasi kidogo cha kodi.
Baada ya miezi kadhaa nilifatilia mkopo benki na nikafanikiwa kupata hivyo nikaongeza mzigo mara kumi zaidi ya ule nilioanza nao.
Sasa nimesikia kwamba maafisa wa tra wanapitia biashara zote na kurudia kufanya makadirio upya kutokana na hali watayoikuta kwenye biashara , majirani zangu wanahaha kufunga maduka yao na kuficha mizigo kwa kuhofia kuongezewa kiwango cha kodi wanayolipa.
Na mimi kabla ya kufanya chochote nikaona ni vyema nipate ushauri wa kutosha kutoka kwa wadau wenye uelewa mzuri juu ya mambo haya ili nijipange vyema kujitetea kufanya wanachofanya wenzangu endapo itabidi. Na ninachotaka kujua hasa ni je ? Wakati wa ukadiriaji wa kodi, biashara inayoendeshwa kwa mtaji wa mkopo inachukuliwaje?
Natanguliza shukrani.